WIZARA YA MAJI KUWACHUKULIA HATUA WAKANDARASI WA MAJI.

MHANDISI KUNDO MATHEW

Wizara ya Maji imeanza kuchukuwa hatua kwa Wakandarasi wanaoshindwa kukamilisha kwa wakati Ujenzi wa Miradi ya Maji kwa Wananchi.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ametoa kauli hiyo wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi ya Maji, huko chemba Mkoani Dodoma.

Aidha, Waziri Kundo amesema Serikali imeendelea kutoa Fedha kwa ajili ya kusogeza huduma za Maji Karibu na Makazi ya Wananchi.

Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Chemba Mkoani Dodoma, wameishukuru Serikali kwa kuimarisha huduma za maji maeneo ya Pembezoni.

Ujenzi wa Miradi ya Maji unaoendelea Nchini, yakiwamo maeneo ya Makazi ya Raia huko pembezoni, ni kielelezo cha utii wa maagizo ya Rais wa Serikali ya Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuhitimisha kero ya Maji kwa akina Mama hao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.