Habari

ZEC YAANZA KUGAWA VITAMBULISHO VYA WAPIGA KURA WAPYA

    Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanza kugawa Vitambulisho vya Wapiga Kura kwa Wapiga Kura Wapya walioandikishwa Mwaka 2023 na 2024. 

    Ugawaji huo Umefanyika katika Vituo mbali mbali vilivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi  Unguja na Pemba.

   Maafisa Uandikishaji wa Tume hiyo Ndg.Khadija Mohamed Ali na Ramadhan Bakari wamesema Zoezi hilo limekwenda vizuri kutokana na Wananchi kupata muamko na kujitokeza kwa wingi kuchukua Kadi zao.

WANANCHI MKOANI NJOMBE WAHAMASIKA KUTAFUTA MSAADA WA KISHERIA

    Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayoenda kwa Jina la “Mama Samia Legal Aid” imezinduliwa Rasmi Mkoani Njombe ambapo Wananchi wa Mkoa huo wametakiwa kuitumia vyema nafasi hiyo ili kukutana na Mawakili wabobevu watakao zunguka katika maeneo yao kwa ajili ya kutatua matatizo  yanayowakabiri ikiwemo migogoro ya ardhi mirathi na ndoa.

MAAFISA UTUMISHI WATAKIWA KUTHAMINI MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA

    Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambae pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo amewataka Maafisa Utumishi kuhakikisha wanajali na kuthamini maslahi ya Watumishi wa Umma kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ari na ufanisi wanapokua katika Majukumu yao.

DC UKEREWE ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA ZANA HARAMU ZA UVUVI KUZISALIMISHA

   Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Christopher Ngubiagai ametoa Siku 14 kwa Wananchi wanaomiliki zana haramu za Uvuvi zinazotumika kuvulia Samaki ndani ya Ziwa Victoria kuzisalimisha mara moja, sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria Watumishi wa Serikali wanaoshirikiana na Wavuvi haramu kuhujumu mapato ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

    Agizo hilo la Serikali limetolewa katika Kikao cha Wadau wa Sekta ya Uvuvi Wilayani humo, kufuatia kushamiri wa vitendo vya Uvuvi haramu unaotishia kupungua kwa Samaki ndani ya Ziwa Victoria.

WAZIRI SHARIFF AAPISHWA KUWA MJUMBE WA TUME YA MIPANGO ZANZIBAR

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mhe.Sharrif Ali Sharrif kuwa mjumbe wa Tume ya Mipango ya Zanzibar

    Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Ikulu Zanzibar kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tume hio ya  Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane.

    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah walishiriki ikiwa ni Wajumbe kutokana na nafasi zao za Uongozi [Vyeo].

UWT MKOANI LINDI WAUNGANA NA RAIS SAMIA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI

     Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mtama mkoani Lindi, ameendesha zoezi la  harambee kwa lengo la kupata nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake katika Halmashaur ya Mtama

     Hii ni kutokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan , kuwa Viongozi wa Chama wanatakiwa wawe na nyumba Kwa ajili ya makazi

WAHITIMU WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUTAFUTA FURSA ZA MASOMO

    Kamishna wa Polisi Zanzibar CP.HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wanafunzi wanaomaliza masomo nchini wasijiingize kwenye makundi ya kihalifu na badala yake watumie fursa za kimasomo zinazotolewa na nchi mbalimbali kupitia mtandao ili kujiendeleza Zaidi na Masomo.

    Akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi katika Mahafali ya Mwaka 2024 ya Skuli ya Feza Zanzibar amesema ni vyema kwa vijana hao kuwa na maadili mema, waaminifu na waadilifu kwani Taifa lina matarajio makubwa kutoka kwao.

TANZANIA YADHAMIRIA KUENDELEZA AMANI NA USALAMA WA BARA LA AFRIKA

     Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania ni kuendeleza na kukuza amani na usalama wa Bara la Afrika ili kujenga ustawi wa Watu wa Bara hilo. 

SMZ NA TAASISI YA SAZANI TRUST KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI

    Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inathamini juhudi za Wadau wa maendeleo wanaounga mkono mapambano dhidi ya udhibiti wa ajali za Barabarani Nchini ambapo hatua hiyo inatachangia ukuaji wa Maendeleo Nchini .

    Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt.Aboud Suleiman Jumbe amesema mapambano ya ajali za Barabarani yatachangia ukuaji wa Maendeleo ya Nchi kwani ni moja ya chachu ya maendeleo. 

SMZ KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO YA SOKA ZANZIBAR

      Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeeleza dhamira yake ya kuanzisha Mfuko wa maendeleo ya soka Zanzibar ili kuendeleza Sekta ya Michezo Nchini.

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameeleza hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf), Dk.Patrice Motsepe na Ujumbe alioongozana nao na kuomba ushirikiano na Caf katika kuzikuza na kuziendeleza Taasisi za Michezo zikiwemo Skuli za Michezo

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.