Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inathamini juhudi za Wadau wa maendeleo wanaounga mkono mapambano dhidi ya udhibiti wa ajali za Barabarani Nchini ambapo hatua hiyo inatachangia ukuaji wa Maendeleo Nchini .
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt.Aboud Suleiman Jumbe amesema mapambano ya ajali za Barabarani yatachangia ukuaji wa Maendeleo ya Nchi kwani ni moja ya chachu ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya SAZANI TRUST Ndg.Safia Mkubwa amesema lengo la kuanzisha kwa Kampeni hiyo ni kuondosha ajali za Barabarani zinazotokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzembe unaofanywa na Madereva ukosefu wa Elimu na kutozingatia sheria za Barabarani.
Katika Kampeni hiyo Wadau mbalimbali wakiwemo wa Usalama Barabarani wamesema wataendelea kushirikiana na Serikali na Wadau ili kumlinda Mtumiaji wa Barabara dhidi ya Ajali zinzotokea.