Habari

MWENGE WA UHURU WATUA LINDI KUTEMBELEA MIRADI 53

      Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo, Mei 24, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa  mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ambapo unatarajia kuweka mawe ya msingi , kuweka ma we ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 45.9
      Makabidhiano ya Mwenge huo  yamefanyika katika viwanja vya Ndege Wilayani Kilwa Mkoani Lindi na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali sambamba na wananchi wa maeneo hayo

SMZ KUFANYA UWEKEZAJI WA WATAALAMU NA MADAKTARI BINGWA KATIKA HOSPITALI MPYA NCHINI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kufanya Uwekezaji Mkubwa wa Wataalamu na Madaktari Bingwa kwenye Hospitali Mpya za Wilaya na Mikoa Nchini.

    Akizungumza Ikulu Jijini Zanzibar na Daktari Suzan Homeida, Raia wa Sudan anayefanyia kazi zake Nchini Rwanda Amesema hatua hiyo ni katika ili kuwapunguzia gharama kubwa Wananchi wanaofuata Matibabu nje ya Nchi hasa kwa maradhi ya Moyo, Saratani,  Uti wa Mgongo na Ubongo.

MAHAKAMA KUU TANZANIA YAFUNGA MKATABA UJENZI WA KITUO CHA UTOAJI WA HAKI

     Mahakama Kuu ya Tanzania na Kampuni ya M/S Deep Construction Limited ya Morogoro imetiliana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Kituo Jumuishu cha utoaji haki Kisiwani Pemba.

     Akizungumza mara baada ya kuweka Saini hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mhe.Kai Bashiru Mbarouk amesema Kituo hicho kitakuwa na mazingira bora ya utendaji kazi na kuwapunguzia shida Wananchi wa Kisiwa cha Pemba kufuata huduma za Kimahakama katika Maeneo ya mbali

UJENZI WA KITUO CHA UMEME URAMBO ASILIMIA 92 ZAFIKIWA

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhe. Gissima Nyamo-Hanga ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa kituoa cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Uhuru - Urambo ( Kilovolti 132) mkoani Tabora ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Doto Biteko aliyoyatoa Machi 27, 2024  alipotembelea mradi huo na kusisitiza usimamizi wa karibu ili kuhakikisha  mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa

WALIMU WATAKIWA KUFUATILIA TAARIFA ZA WANAFUNZI ILI KUKOMESHA VITENDO VYA UNYANYSAJI WA WATOTO

    Mkaguzi kata ya Mnyanjani Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/IVil, Faharia Massala akifuatilia Mienendo ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Kwanjeka Wilaya ya Tanga jiji, Mkoa wa Tanga amewaomba walimu kuhakikisha wanafuatilia na kupata taarifa za wanafunzi hao ili kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa Watoto hao.

     Mkaguzi huyo ametoa rai hiyo shuleni hapo ambapo amebainisha kuwa watoto hao wanapaswa kupewa malezi na kufuatiliwa kwa karibu kutokana na vitendo vya baadhi ya watu wasio na maadili kuwafanyia watoto ukatili.

SERIKALI YAAHIDI KUTOA KIWANJA UJENZI OFISI ZA MAHUJAJI SAUDI ARABIA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameahidi Serikali kutoa kiwanja kwa ajili ofisi za kudumu za Mahujaj wanaojiandaa kwenda kushiriki ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia.

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya kuwaaga Mahujaj wanaokwenda ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia iliyofanyika Msikiti wa Jaamiu Zinjibar Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 23 Mei 2024.

SERIKALI KUTOA FURSA KWA VIJANA KATIKA SEKTA YA UJENZI

       Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) pamoja na Bodi ya Usajili wa Wakadiriaji Majenzi na Wabunifu Majengo (AQRB) kuandaa mpango mahsusi wa kuwajengea uwezo vijana kwa nyenzo na ujuzi ili waanzishe Makampuni ya Ujenzi na Ushauri Elekezi zitakazoshiriki katika ujenzi wa miundombinu.

MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 65 KUKAGULIWA NA MWENGE MKOA KUSINI UNGUJA

Mwenge wa Uhuru umeanza Mbio zake katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Miradi Kumi na moja yenye Thamani ya zaidi ya Shiling Bilioni Sitini na Tano itakagukiwa na kuzinduliwa na kuwekewa Jiwe la Msingi.

Akipokea Mwenge huo ukiotokea Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Mwenge utakimbizwa Kilo 177 ndani ya Mkoa huo na kuipita Miradi mbali mbali ya kimkatiti ambayo inalengo la kutatua matatizo yanayowakabili Wananchi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA MAZINGIRA WEZESHI KWA VYOMBO VYA HABARI.

 Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa, amezitaka Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Habari Nchini, kuimarisha Mazingira wezeshi kwa Waandishi wa Habari za Mitandaoni, ili kufikia uchumi wa Kidijitali.

 akizungumza katika Kongamano la Wamiliki wa Vyombo vya Habari za Mtandaoni, Mhe Kassim amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau wa habari za Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari, ili kuharakisha ukuaji wa maendeleo Nchini.

WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUNUFAIKA NA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Khadija Khamis Rajab amesema Wizara ina Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za gharama Nafuu na Biashara ambazo zimewalenga zaidi WANANCHI wa kipato cha chini ili kukidhi mahitaji.

Akizungumza katika muendelezo wa Ziara zake na kuangalia maeneo ambayo Serikali inatarajia kujenga Nyumba za gharama nafuu na Biashara katika maeneo ya Kibele, Dunga, Mwera, Kitogani na Chumbuni.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.