Habari

WASIMAMIZI WA UTOAJI NA USAFIRISHAJI WA MIZIGO KUWEKA MIKAKATI ILI KUPUNGUZA UPOTEVU WA MALI.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Khalid Salum Mohammed amewataka Wadau na Wasimamizi wa utoaji  na usafirishaji wa Mizigo  CAGO kuweka Mikakati itakayopunguza athari zinazosababisha Maafa na upotevu wa Mali.

Akifungua Mkutano wa Wadau wa usalama wa Anga na Wanaosafirisha na  wanaotoa Mizigo  katika Nchi za Afika Dkt Khalid amesema hivi sasa dunia inaenda Kidigitali hivyo usalama wa Mizigo ni muhimu ambapo Mafunzo hayo yatayawezesha kutambua wanaosfirisha mizigo kwa njia zisizo Halali.

ZAIDI YA MAGUNIA 80 YA MAKONYO YAMEKAMATWA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI

Zaidi  ya Magunia 80 na Unga wa Makonyo yamekamatwa katika harakati za kusafirishwa kwenda nje ya Nchi kinyume na taratibu katika Shehia ya Msuka Wilaya ya Micheweni.

Akizungumza Kitendo hicho cha uhujumu wa Uchumi  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini   Pemba Salama Mbarouk Khatib amewataka wafanya biashara kufuata taratibu kulingana na Vibali vyao wanavyoomba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la biashara la Taifa Zanzibar ZSTC Soud Saidi Ali   amesema Serikali haijatoa ruhusa kwa Wananchi kusafirishwa Bidhaa zinazotokana na karafu kwenda Nje ya Nchi..

WIZARA YA UCHUMI WA BLUU KUFANYA UTAFITI WA SUMU YA KASA

    Wizara ya Uchumi wa Bluuu na Uvuvi   imepanga kufanya utafiti juu ya Sumu Asili ambayo imo ndani ya Mwili wa Kasa. 

imesema  imeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuzitambua Sumu  zilizomo ili kujua athari zake . 

    Akijibu Swali la  Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani  Mhe.Mussa Foum Mussa  Waziri wa Wizara hiyo amesema  Elimu itakayopatikana kutokana na utafiti huo itatumika katika kuelimisha Jamii juu ya athari zitonazo na ulaji wa Kasa . 

WATANZANIA WAFANYA KUMBUKIZI YA MIAKA 28 YA AJALI YA MELI YA MV. BUKOBA

    Watanzania leo wamefanya kumbukizi ya Miaka 28 ya Ajali ya Meli ya Mv. Bukoba iliyotokea Mwaka 1996 katika Ziwa Victoria, huku baadhi ya Wananchi waliopoteza Ndugu na Jamaa zao katika ajali hiyo wakiiomba Serikali kuienzi Siku hiyo na kuimarisha usalama wa Vyombo vya Majini.

    Kumbukizi hiyo imefanyika katika Makaburi ya baadhi ya Waliofariki katika Ajali ya Mv. Bukoba yaliyopo Igoma Jijini Mwanza.

Paroko wa Parokia ya Nyamhongolo Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Padri George Nzugu ameongoza Sala ya kuwaombea Marehemu hao.

MAHKAMA KUU ZANZIBAR YATILIANA SAINI NA UBALOZI WA SWITZERLAND

    Mahkama Kuu Zanzibar imetiliana Saini na Ubalozi wa Nchini Tanzania Switzerland juu ya muongozo wa kutaifisha mali ambazo zimepatikana kwa njia ya uhalifu.

    Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdallah amesema Utiaji Saini huo ni utaratibu wa kuzitaifisha mali ambazo zimepatikana kwa njia ya uhalifu na kuhakikisha Mhalifu halipwi kwa mujibu wa Sheria zilizopitiwa katika Mkataba huo miongoni mwa Sheria hizo ni Sheria za Dawa za Kulevya , mwenendo wa makosa ya Jinai na sheria za KMKM.

SMZ HAIJAFANYA MABADILIKO YOYOTE YA BEI ZA MALIASILI ZISIZOREJESHEKA

      Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema haijafanya mabadiliko yoyote ya Bei za Maliasili zisizorejesheka kwani kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Madereva kusingizia ugumu wa upatikanaji wa vibali na kuwalangua Wananchi. 

     Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema hayo  wakati akitoa Taarifa ya Ufunguzi wa Shimo jipya la Mchanga kwa shunguli za Ujenzi amesema vibali vyote vya uombaji vinapatikana kupitia Mtandao hivyo amewasisitiza Wananchi anaepaswa kuomba vibali yule anaehitaji rasilmali hiyo.

WAZIRI MKUU AKUBALI KUWA MITANDAO YA KIJAMII INA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA

      Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mei 21, 2024 ni mgeni rasmi katika kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) na kuipongeza kwa kuwa na mchango wa Maendeleo ya Taifa.

Katika Kongamano hilo, yamejadiliwa mambo kuhusu miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Madarakani pamoja na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Viongozi wengine wanaoshiriki katika kongamano hilo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi.

WAZIRI HAROUN KUIMARISHA MIFUMO YA KIELETRONIC KWA WATUMISHI WA UMMA.

Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria Utumishi na Utawala bora imesema Mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kutekeleza Bajet yake kwa kuzingatia vipaumbele vya kuendeleza Mifumo ya Kieletrpnic katika Utumushi wa Umma na kusimamia misingi ya Utawala bora.

Akiwasilisha Hutuba ya Makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo Waziri wa Wizara hiyo Mh Haruna Ali Sleimain amesema kufanya hivyo kutasaidia Kuimarisha vipaumbele vyengine  ikiwemo kusimamia misingi ya maadili, kuongeza  mapambano zidi ya Rushwa  pamoja na ukaguzi na udhibiti wa Rasilimali za Umma.

MAKAMU WA RAIS AMETOA MAAGIZO KUIMARISHA SEKTA YA ASALI NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Philip Mpango, ametoa maagizo mbalimbali   yatakayosadia kuimarisha sekta ya asali Nchini ikiwemo Balozi zote kujidhatiti kutafuta Masoko ya Bidhaa zinazotokana na Nyuki ili kusaidia Taifa kupata Fedha za Kigeni na kujimarisha Kiuchumi.

Dk.Mpango ametoa  maagizo hayo  wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma.

Aidha Dkt.Mpango ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta hiyo kuja na mpango maalum wa Ufugaji wa Nyuki.

VYAMA VYA UKOMBOZI CCM NA CPC KUIMARISHA UHUSIANO

Ujumbe wa Chama cha ukombozi nchini china cpc umefanya ziara maalum ya kisiasa kwa ajili ya kuimarisha umoja kati ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi CCM

Akizungumza na ujumbe huo huko Ofisi Kuu ya Chama Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mohammed Said Dimwa amesema Ziara hiyo itaongeza ushirikiano kati yao hasa katika kuongeza nguvu ya Chama

Mwenyekiti wa Maskani Kaka Kisonge Dk Juma Rajab Juma amepongeza kuja kwa Ujumbe huo ambao utasaidia kubadilishana uzowefu katika kuvitumikia Vyama hivyo pamona na kujenga Demokrasia ndani ya chama

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.