Habari

ZANZIBAR IMESISITIZWA KUTILIA MKAZO ELIMU YA MAFUNZO YA AMALI

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Eastern Mediterranian cha Uturuki umeishauri Zanzibar kutilia mkazo Elimu ya Mafunzo ili kuwawezesha Vijana kupata Taaluma inayoendana na mazingira yao.

Wakizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali huko Mazizini Uongozi huo ulioambatana na Mkuu wa Chuo hicho Professa Hassan Kiliic kujitambulisha wameseha hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar  kuyafikia mageuzi ya Elimu.

SAINI MAZRUI UNICEF

Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana Saini na UNICEF Mkataba wa Manunuzi wenye Thamani ya Dola Milioni 12 na Laki Tano sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni Thelathini kupitia Mradi wa uwekezaji wa huduma ya Mama na Mtoto unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

POLISI WANAWAKE MKOA WA ARUSHA WAMETAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VINAVYOKWENDA KINYUME JESHI HILO

     Katibu wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania TPF net Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Pili Mande amewataka Askari wa kike Mkoa wa Arusha kujiepusha na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya Jeshi hilo.

     Kauli hiyo ameitoa leo wakati akitoa mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao huo kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Askari wa kike Jijini humo ambapo amewataka kutambua malengo mazuri ya kuanzishwa kwa mtandao huo.

WAZIRI NAPE AWASISITIZA WAZAZI KUTOWAACHA WATOTO KULELEWA NA MITANDAO

      Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesisitiza kwa wazazi wasiache watoto kujikita zaidi na mitandao katika mambo yasiyofaa kuliko kujifunza.

WATUMIAJI WA BAHARI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA KIMBUNGA "IALY"

     Kufuatia taarifa iliyotolewa tarehe 17 Mei 2024 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu kuwepo kwa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar, Mamlaka inapenda kutoa mrejeo kuhusiana na mwendendo wa kimbunga hicho.

      Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kimeendelea kuimarika na bado kimeendelea kusalia katika Bahari ya Hindi kama ilivyotabiriwa awali, hadi ilipofika saa 3 asubuhi ya leo kilikuwa umbali wa takriban kilomita 680 mashariki mwa pwani ya nchi yetu.

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA ZAIDI YA MIRADI 23 KATIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

     Jumla ya miradi 23 ya zaidi ya Billion 5 inatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Kitaifa wa Uhuru 2024 kwa Mkoa wa Mjini Magharibi.

    Akizungumza katika mapokezi ya Mwenge huo huko Uwanja wa Ndege Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrissa Kitwana Mustafa amesema mbio za Mwenge wa uhuru, Mkoani humo zitahusisha kilomita 104 na kutembelea miradi 23 ya maendeleo.

SUZA YATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT)

      Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimetiliana Saini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakilenga uimarishaji wa Sekta ya Elimu katika masuala ya Utalii na kukuza Sekta hiyo.

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YA ANGA

     Mkurugenzi Mkuu wa Anga Kenya Emile Ngunza Arao amesema mazingira raifiki yaliyowekwa katika Sekta hiyo Nchini humo, yamekusudia kuwawezesha Wwananchi kutumia Usafiri wa Anga.

     Akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kufunga Kongamano la Sita la Usafiri wa Anga la Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema moja ya uimarishaji huo ni kupunguza Bei ya Tiketi ili kuwezesha Wananchi wa Vipato vyote kumudu gharama za usafiri wa Anga.

WANAFUNZI WA ZANZIBAR KUPATIWA FURSA ZA MASOMO NCHINI POLAND

      Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohammed Mussa amesema Wizara hiyo itahakikisha inawatafutia Wanafunzi wenye fursa za kusoma Nchi mbalimbali ili kuona wanapata taaluma zitakazowasaidia katka kuleta maendelo ya Nchi. 

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Mh.Lela amesema amepokea ujio wa Balozi wa Poland aliyekuja kwa lengo la mahusiano katika Sekta ya Elimu ya juu kwa Poland na Zanzibar ili Wanafunzi wa Zanzibar wapate ufadhili wa kusoma fani tofauti ambazo zinaenda na sayansi na teknolojia. 

VYAMA VYA SIASA VIMEOMBA KUTEKELEZWA KWA VITENDO WANAYOKUBALIANA

    Viongozi wa Vyama vya Siasa wameomba kutekelezwa kwa vitendo falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza Demokrasia Nchini kwa kuhakikisha hakuna mkwamo wa Kisaiasa kwa maslahi ya Wananchi.

    Viongozi wa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini wanaokutana Zanzibar kwa Siku Mbili katika Kongamano la Demokrasia, wamesema iwapo falsafa hiyo inayohusisha mambo Manne yatafanyiwa kazi yakiwemo ya maridhiano, ustahamilivu na mageuzi ya Demokrasia, itawezesha kufikiwa maridhiano ya Kisiasa Tanzania na kukuza ustawi wa maendeleo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.