ZANZIBAR IMESISITIZWA KUTILIA MKAZO ELIMU YA MAFUNZO YA AMALI

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Eastern Mediterranian cha Uturuki umeishauri Zanzibar kutilia mkazo Elimu ya Mafunzo ili kuwawezesha Vijana kupata Taaluma inayoendana na mazingira yao.

Wakizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali huko Mazizini Uongozi huo ulioambatana na Mkuu wa Chuo hicho Professa Hassan Kiliic kujitambulisha wameseha hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar  kuyafikia mageuzi ya Elimu.

Wamesema Zanzibar ni Kisiwa chenye fursa za kutosha, hivyo Elimu ya vitendo itawasaidia Vijana kutumia vizuri fursa zilizowazunguka

Akizungumzia ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Chuo hicho cha Uturuki, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela mohammed Mussa amesema Chuo cha Eastern Mediteranian kitaweza kuwaongezea ujuzi wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar na kuongeza ufanisi wa Taaluma

Mh Lela amesema Uturuki imepiga hatua katika Elimu ya vitendo hivyo ushirikiano huo utaisaidia Zanzibar katika Elimu ya vitendo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.