SMZ HAIJAFANYA MABADILIKO YOYOTE YA BEI ZA MALIASILI ZISIZOREJESHEKA

Waziri Kaduara

      Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema haijafanya mabadiliko yoyote ya Bei za Maliasili zisizorejesheka kwani kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Madereva kusingizia ugumu wa upatikanaji wa vibali na kuwalangua Wananchi. 

     Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema hayo  wakati akitoa Taarifa ya Ufunguzi wa Shimo jipya la Mchanga kwa shunguli za Ujenzi amesema vibali vyote vya uombaji vinapatikana kupitia Mtandao hivyo amewasisitiza Wananchi anaepaswa kuomba vibali yule anaehitaji rasilmali hiyo.

    Pamoja na mambo mengine Waziri Kaduara amesema hakuna Soko la Mchanga na Maliasili nyengine katika eneo la Taveta na Maeneo mengine Nchini hivyo Gari itayobainika inafanya shunguli hizo sheria itachukuliwa dhidi yake .

    Wizara ya Maji Nishati na Madini imelifunga Shamba la Talib Hamad Omar lililopo Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini 'a' Unguja kutokana na kumalizika kwa Mchanga unaofaa kwa Shunguli za Ujenzi na kulifungua Shamba la Aziz Khamis Aziz lililopo Donge Mchangani Wilaya ya Kaskazini 'a' Unguja kwa ajili ya kutoa huduma kwa Miradi na Jamii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.