Wizara ya Uchumi wa Bluuu na Uvuvi imepanga kufanya utafiti juu ya Sumu Asili ambayo imo ndani ya Mwili wa Kasa.
imesema imeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuzitambua Sumu zilizomo ili kujua athari zake .
Akijibu Swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani Mhe.Mussa Foum Mussa Waziri wa Wizara hiyo amesema Elimu itakayopatikana kutokana na utafiti huo itatumika katika kuelimisha Jamii juu ya athari zitonazo na ulaji wa Kasa .
Amesema Wizara inaendelea kuchukua hatua kwa Wavuvi ambao wanaendelea kujishughulisha na Uvuvi wa Viumbe hao.
Wakati huo huo Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe.Shamata Shaame Khamis amesema Kilimo cha Kisasa kina mchango mkubwa wa kuwakomboa Wakulima iwapo maeneo yatapatiwa Teknolojia za Kisasa kwa kuzalisha Mazao yenye tija kwa Eneo Dogo.
Wajumbe wa Baraza la Wawaakilishi wamepitisha Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais ,Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.