Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kufanya Uwekezaji Mkubwa wa Wataalamu na Madaktari Bingwa kwenye Hospitali Mpya za Wilaya na Mikoa Nchini.
Akizungumza Ikulu Jijini Zanzibar na Daktari Suzan Homeida, Raia wa Sudan anayefanyia kazi zake Nchini Rwanda Amesema hatua hiyo ni katika ili kuwapunguzia gharama kubwa Wananchi wanaofuata Matibabu nje ya Nchi hasa kwa maradhi ya Moyo, Saratani, Uti wa Mgongo na Ubongo.
Amesema Zanzibar inahitaji Ushirikiano wa kina kwa Madaktari Bingwa na Wataalamu kwa Maeneo Manne ya Afya ikiwemo Upasuaji wa Moyo, Saratani, Mfumo wa Mishipa ya Fahamu inayohusisha Uti wa Mgongo na Ubongo.
Hivyo Dk.Mwinyi amemuomba Dk.Suzan kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwapata Wataalamu na Madaktari Bingwa na wa Kawaida kutoka Sudan ili kuongeza nguvu kwa Hospitali ya Mkoa ya Lumumba za Wilaya Nchini kote kwa maendeleo ya Sekta ya Afya.
Daktari Suzan Homeida ameahidi kushirikiana na Serikali ili kuendeeza Sekta ya Afya Nchini.
Dk.Suzan ni Daktari Mshauri Mkuu wa Magonjwa ya Damu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya “Frontierpoly21” iliyopo Mjini Kigali na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Teknolojia Mjini Khartoum, Sudan.
Katika hatua nyengine Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Kapteni Hussein Mohammed Seif kuwa Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibara KMKM.