MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 65 KUKAGULIWA NA MWENGE MKOA KUSINI UNGUJA

MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA

Mwenge wa Uhuru umeanza Mbio zake katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Miradi Kumi na moja yenye Thamani ya zaidi ya Shiling Bilioni Sitini na Tano itakagukiwa na kuzinduliwa na kuwekewa Jiwe la Msingi.

Akipokea Mwenge huo ukiotokea Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Mwenge utakimbizwa Kilo 177 ndani ya Mkoa huo na kuipita Miradi mbali mbali ya kimkatiti ambayo inalengo la kutatua matatizo yanayowakabili Wananchi.

Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Godfrey Elyakim Mnzava amesema Serikal imewekeza Miradi katika maeneo ya uwekezaji ili kuimarisha Sekta ya Biashara jambo litakalowawezesha Wananchi kunufaika Kiuchumi.

Jumla ya Miradi 6 imekaguliwa na Mbio za Mwenge Wilaya ya kati ikiwemo Ujenzi wa Barabara Dunga Zuze, Tanki Tangi la Maji safi na salam, aujenzi wa Skuli Mwera, Ujenzi wa Nyumba za Madaktari Mwera Pongwe, Soko la Wajasiriamali Kikungwi, pamoja na kushiriki shughuli ya upandaji Miti Jozani.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.