TANZANIA YADHAMIRIA KUENDELEZA AMANI NA USALAMA WA BARA LA AFRIKA

DKT.SAMIA

     Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania ni kuendeleza na kukuza amani na usalama wa Bara la Afrika ili kujenga ustawi wa Watu wa Bara hilo. 

   Raisi Dkt.Samia amesema hayo wakati akifungua maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC-AU) yaliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema jitihada za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazolikabili Bara la Afrika na katika kukuza maendeleo ya Kijamii na kiuchumi ndani ya Bara la Afrika.

    Amesema Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha Bara la Afrika linafikia malengo iliyojiwekea ambapo amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika kwa tathmini ya safari ya uwepo wa chombo hiki tangu kilipoanzishwa hadi sasa na mikakati inayopaswa kuwekwa ili kufikia Afrika tuitakayo.

    Akizungumzia suala la Ugaidi ndani ya Bara la Afrika Raisi Samia amehimiza umuhimu wa kutafakari kuhusu namna ya kushughulikia changamoto hiyo na kusistiza suala la ushirikiano na Wadau wa kikanda ili kupata utaalamu na rasilimali zitakazolisaidia Bara la Afrika.

   Awali  Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Mahamat Moussa Faki amesistiza umuhimu wa kufuatwa kwa mifumo ya kisheria, uwazi katika kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi yanayofikiwa kwa ufanisi.

    Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema ni muhimu kuwa na jitihada za pamoja ili kufikia dhamira ya kuwa na afrika yenye amani na umoja.

    Kongamano hilo la Ngazi ya juu la kumbukizi ya Miaka 20 liliambatana na Midahalo iliyowajumuisha Viongozi Wakuu Wastaafu wa Bara la Afrika   ambao wameeleza umuhimu wa kuwa na chombo hicho chenye jukumu la kuzuia, kudhibiti na kutatua Migogoro ndani ya Bara la Afrika.                    

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.