Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mhe.Sharrif Ali Sharrif kuwa mjumbe wa Tume ya Mipango ya Zanzibar
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Ikulu Zanzibar kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tume hio ya Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah walishiriki ikiwa ni Wajumbe kutokana na nafasi zao za Uongozi [Vyeo].
Mhe.Sharrifa Ali Sharrif ambae ameapishwa kuwa ni Mjumbe ndani ya Tume hio ya Mipango,Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji.
stories
standard