Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameeleza hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf), Dk.Patrice Motsepe na Ujumbe alioongozana nao na kuomba ushirikiano na Caf katika kuzikuza na kuziendeleza Taasisi za Michezo zikiwemo Skuli za Michezo
Amesema, Zanzibar inajivunia hatua ya Sekta ya Michezo ilivyofikiwa kwa kuimarika miundombinu ya kisasa na kuahidi Serikali kufanya makubwa zaidi kuimarisha miundombinu ya Michezo .
Dkt. Motsepe amesifu juhudi za Serikali kwa hatua ya kuinua Sekta ya Michezo na maendeleo makubwa yaliyofikiwa Zanzibar ikiwemo kuwa na uwanja mpya wa michezo “New Aman Complex” wenye hadhi ya Kimatafa na kukidhi viwango vyote vya Fifa.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Damas Daniel Ndumbaro amesema, kuelekea Afcon 2027, Tanzania inatarajiwa kuwa na Viwanja 11 nyenye kukidhi sifa zote za Viwanja vya Kimataifa baada ya kufanyiwa matengenezo vikiwemoVvitatu Zanzibar.
Akizungumzia Fainali za Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika kwa Skuli za Caf, Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema, Serikali imetimiza wajibu wake kwa kuweka mazingira yote salama kwa Fainali hizo.
Fainali za Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika za Caf zinafanyika chini ya udhamini mkubwa wa “Motsepe Foundation” ambayo zimewashirikisha Wachezaji chini ya Miaka 15 kutoka Mataifa 11 ya Afrika