RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA NCHINI KOREA .

JANUARY MAKAMBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya Ziara ya kikazi ya siku 6 Nchini Korea ikiwa ni mwaliko wa wenyeji wake Rais wa Taifa hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Mkamba amesema ziara hiyo inatarajiwa kuanza May 30 hadi Juni 6 mwaka huu ambapo pia Rais Dkt Samia anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Korea.

Pia Waziri Makamba amesema katika Ziara hiyo Rais Samia anatarajiwa kutunukiwa Shahada ya heshimu ya PHD na Chuo Kikuu cha masuala ya Anga Korea Aerospace (Kau)

Katika ziara hiyo Tanzania inatarajia kusaini Mikataba Saba na Jamhuri ya Korea itakayojikita katika Sekta za Madini, Elimu, Usafiri wa Anga, Uchumi wa Blue, hati ya makubaliano ya Tamko la pamoja la Kisiasa, utambuzi wa Vyeti vya pamoja na Mkataba wa Kifedha kati ya Exim ya Korea na Tanzania                                       

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.