Wizara ya Afya imesema huduma za Mfuko wa Bima ya Afya Zanzibar hazipatikani katika baadhi ya Hospitali kutokana na Hospitali hizo kutokukidhi vigezo vya kutoa huduma kwa Wnachama wake.
Naibu waziri wa Wizara hiyo Mh Hassan Khamis Hafidhi amesema sababbu nyengine zinatokana na kuwepo kwa upunbgufu wa Madaktari, Dawa pamoja na kutokuwa na Vifaa Tiba katika baadhi ya Hospitali.
Amesema kupitia Udhamini wa Shirika la maendeleo la Ujerumani Mfuko huo pia unatarajiwa kufanya kazi ya usajili wa makundi tofauti.
Wakati huo huo Serikali imesema itaendelea na Mikakati ya kuzijenga Bandari za Unguja na Pemba ili kufikia Malengo ya kuwaletea Maendeleo ya Kiuchumi Wananchi wake.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Mh Nadir Abdulatif amesema Azma ya Serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wananchi kwa kuwasogezea Maendeleo ya haraka kupitia Ujenzi wa Miundombinu ya Babarabara, Bandari na Viwanja vya Ndege.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo umwagiliaji Maliasili na Mifugo.
BAADHI YA HOSPITALI HAZINA SIFA YA HUDUMA YA MFUKO WA BIMA YA AFYA
stories
standard