Katika kuadhimisha Siku ya Hedhi Salama Duniani Wanawake wametakiwa kuzidisha usafi kwenye kipindi hicho ili kujinga na magonjwa mbalimbali yanayoweza kujitokeza.
Ushauri ho umetolea na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kinamama Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Dk.Fatma Said Mohamed wakati akizungumza na ZBC katika Siku ya Hedhi Salama Duniani.
Amesema katika Kipindi cha Hedhi Wachina na Wanawake wanakuwa katika mazingira hatarishi ya kupata Magonjwa mbali mbali yakiwemo ya Fangasi hivyo wanapaswa kuwa katika mazingira ya usafi ili kuepukana na Magonjwa yanayoweza kujitokeza.
Aidha amesema katika Kipindi hicho baadhi ya Wasichana wamekuwa wakipitia kipindi kigumu na kupelekea kukosa baadhi ya Vipindi vya Masomo huku akiiyomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuweka mazingira rafiki kwa Wanafunzi Wakike.
Akieleza matatizo ya kiafya yanayoweza kujitokeza kwa kukosekana Hedhi salama kwa Wasichana na Wanawake ni pamoja Magonjwa ya Fangasi katika sehemu zao za siri.