Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu (3) mkoani Geita kwa lengo la kushiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira ambapo kikanda yatafanyika mkoa wa Geita, na kimkoa yamepangwa kufanyika wilayani Chato.
Mhe. Waziri Mkuu atazungumza na watumishi na wakuu wa taasisi mbalimbali, Pia atakuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwamo kuweka jiwe la msingi katika soko la samaki Wilayani Chato na baadae atakuwa na mkutano wa hadhara wilayani humo, Wilayani Nyang’hwale ataweka jiwe la msingi katika jengo la halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na kuzindua jengo la uwezeshaji wananchi kiuchumi Kalemwa, Nyang’hwale na kufanya mkutano wa hadhara.
Mheshimiwa Majaliwa atawasili mkoani Geita tarehe 31 Mei, 2024 na atahitimisha ziara yake tarehe 2 Juni 2024 ambapo atetembelea Wilaya tatu za Geita, Wilaya ya Chato na Wilaya ya Nyang’hwale.