Maabara ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)imepata ithibati ya viwango vya ubora wa Kimataifa katika kutoa huduma za Vipimo vya Magonjwa ya moyo na Magonjwa mengine.
Ithibati hiyo iliyotolewa na Shirika la kimatifa la viwango iso kufuatia JKCI kukidhi Vigezo vyote vilivyowekwa na Shirika hilo ikiwemo kuwa na Mashine za kisasa zinazotoa Vipimo zaidi 86 vya Uchunguzi wa Magonjwa mbali mbali yakiwemo ya moyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete (JKCI)Dkt. Peter Kisenge amesema kutolewa kwa ithibati hiyo kunamaanisha majibu ya vipimo vyote vinavyotolewa na Maabara hiyo vinaaaminika popote Duniani .
Dkt. Kisenge amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha Taasisi hiyo kwa Ununuzi wa Vifaa vya Kisasa pamoja na kuwepo Wataalamu wakutosha .
Nae Kaimu Mkuu wa Maabara Emanuel Mgao amesema toka Maabara hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2018 imeweza kukidhi Viwango vya Kimataifa vya utoaji wa huduma bora za Maabara.
Ithibati hiyo imetilewa Tarehe 28/5/2024 kwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI na Shirika la viwango la Kimataifa la ISO.