Habari

WANAFUNZI ELFU TANO KUFANIKIWA KUENDELEA NA MASOMO KIDATU CHA TANO .

Zaidi ya Wanafunzi Elfu Tano wamefanikiwa kuendelea na Masomo yao ya Kidatu cha Tano katika Skuli za Serikali na Binafsi .

Akizungumza  na Waandishi wa habari Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Ali Abdul-Gulam husen amesema Idadi ya ufaulu wa Wanafunzi kwa Mwaka 2023  imeongezeka kwa Asilimia 21 ukinganisha na Matokeo yaliopita jambo ambalo limefanya Wizara kuongeza idadi ya Skuli kutokana na wingi wa Wanafunzi .

KWARARA KIDUTANI WAFAIDIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA. UPSAUND1:WANANCHI

Wananchi wa Kwarara Kidutani wamesema upatikanaji wa Maji safi na salama utasidia kwa kiasi kikubwa kufikia maendeleo ya Wananchi kwa kuwapunguzia usumbufu waliokua nao.

Moja kati  ya changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama ndani ya Kijiji hicho jambo ambako lilikiwa likirejesha nyuma juhudi zao za kujikomboa Kiuchumi.

BALOZI SAID OTHMAN AWATAKA WATANZANIA WAISHIO NCHINI COMORO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA

     Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro amekutana na Watanzania wanaoishi nchini Comoro na kuwaasa wawe mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuitangaza vyema Tanzania katika jumuiya za kimataifa.

     Mheshimiwa Balozi Saidi Yakubu alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa Watanzania na kueleza mikakati yake pamoja na Ubalozi katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro.

ZANZIBAR KUZINDUA MRADI WA UWEKEZAJI WA VISIWA

     Zanzibar inatarajia kuzindua Mradi wa Historia wa Uwekezaji katika Visiwa vidogo vidogo kwa Kisiwa cha Bawe kilichopo mkoa wa Mjini Magharib, ambao umegharimu kiasi cha Dola Milioni 37.

     Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari Katibu Mkuu Wizara Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Ndg.Khamis Suleiman Shibu, amesema Uzinduzi huo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha Uchumi unatarajiwa kufanyika Juni 15 Mwaka huu.

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WATU WENYE ULEMAVU

     Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB) na Jumuiya nyengine za Watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia Watu wenye Ulemavu kufaidika na fursa mbali mbali Nchini.

MAJAALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI WILAYA YA NYANG'HWALE

      Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85.

     Akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo ambapo mpaka sasa limegharimu shilingi bilioni 3.7, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha majengo ya utawala kwenye halmashauri zetu “Lengo la Rais Dkt. Samia ni kuona wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao”.

NAIBU WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUTOBAGUANA KWA TOFAUTI ZA KIDINI NA VYAMA VYA SIASA

     Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kudumisha amani, mshikamano na  upendo na kamwe wasigawanywe kwa sababu yoyote.

     Amesema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Robert Yondam Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji mkoani Mbeya.

WAKAAZI WA NYUMBA ZA MICHENZANI WAILALAMIKIA MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR ( ZAWA )

     Wakaazi wa Michenzani Jumba Namaba Nne wameilalamikia Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA kutokana na kupata Maji Machafu.

    Akizungumza kwa Niaba ya Wenzake Ndg.Juma Saleh Juma amesema hali hiyo hutokea pale Maji yanapofunguliwa baada ya kufungwa.

    Hivyo amesema ni vyema kwa Wahusika kulirekebisha tatizo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo Maradhi ya Mripuko.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUHAKIKISHA BIDHAA ZAO ZINAKIDHI UBORA WA VIWANGO

    Wafanyabiashara wanaoleta Bidhaa kutoka Nje ya Nchi wametakiwa kuhakikisha Bidhaa hizo zinakidhi  vigezo na masharti   ili kuweza kukuza Soko Kitaifa na Kimataifa.

    Akizungumza katika  Mkutano wa Waingizaji wa bidhaa za Uchapishaji Afisa Viwango Kemikali ZBS ,Ndg.Thahiri Khelefu Ali  Amesema  hivi sasa kumekuwa na bidhaa nyingi kutoka Nje zisizokuwa na Vigezo hivyo amewataka  Waingizaji hao kuhakikisha Bidhaa wanazoingiza zinakizi Vigezo ili kuepusha gharama na  usumbufu kwa Watumiaji wa Bidhaa hizo.

RAIS MWINYI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA

     Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza azma yake ya kutaka kusambaza Umeme Vijiji vyote vya Unguja na Pemba na kukuza maendeleo Maeneo hayo.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes aliyekuja kujitambulisha.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.