Habari

MITI ELFU 14KUPANDWA PWANI YA TUMBE MAGHARIBI WILAYA YA MICHEWENI

     Jumla ya Miti Elfu Kumi na Nne (14,000) Aina ya Mikoko imepandwa Shehiya ya Tumbe Magharibi katika Sherehe za kuelekea Maazimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

   Akizungumza Katika Maazimisho hayo , Mkuu wa Wilaya ya Micheweni , Mgeni Khatib Yahya, amesema Serikali inaunga Mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Washirika wa Maendeleo Koica kwa kushirikiana na Wananchi katika Upandaji wa Miti kwa lengo la kuhifadhi Mazingira ,kujikinga na mabadiliko ya Tabia Nchi.

SERIKALI IMESEMA HAIJAWEKA REHANI CHOCHOTE KUPATA MKOPO WA BILIONI 2.5 KUTOKA SERIKALI YA KOREA

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haijatoa wala kuweka rehani kitu chochote kwa ajili ya kupata Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 2 Nukta 5 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea.

WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU KUVALISHWA MIKANDA YA MAWASILIANO
MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA HUKO BANDA MAJI

    Kijana anaefahamika kwa Jina la Nada Faki Khamis Mwenye Umri wa Miaka Thelathini na Nane Mkaazi wa Kinyasini Wilaya ya Kaskazini 'a' Mkoa Kaskazini Unguja amekutwa akielea katika Bwawa la Maji la  Banda Maji  Akiwa Amefariki Dunia 

WATENDAJI WILAYA YA MKOANI WATAKIWA KUWA WAWAJIBIKAJI KATIKA NAFASI ZAO

    Watendaji wa Taasisi za Serikali Wilaya ya Mkoani wametakiwa kufuata Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

    Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja ameyasema hayo katika Kikao kazi na Watendaji wa Serikali Wilayani humo, kiliofanyika katika Ukumbi wa Umoja ni nguvu Mkoani.

   Mjaja amewataka Wafanyakazi hao kila Mmoja kwa Nafasi yake, kusimamia vyema mapato ya Serikali, ikiwemo kudai Risiti za Elektonic kila wanapofanya Miamala ya  Kibiashara.

MAAFISA,WAKAGUZI NA ASKARI WATUNUKIWA NISHANI YA MUUNGANO

    Zaidi ya Maafisa, Wakaguzi na Askari Mia Sita wa Vyeo mbalimbali wametunikiwa Nishani ya Muungano kwa kuthamini umuhimu wao katika kuendeleza Ujenzi wa Taifa 

    Akiwavisha Nishani hizo kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kamanda Mkuu wa Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura amesema Nishani hiyo ni heshima kwao na wanapaswa kujituma zaidi katika kuimarisha Ulinzi na Usalama

WAFANYABIASHARA FUNGU REFU WATAKIWA KUIMARISHA USAFI

    Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Rashid Hadidi Rashid amewataka Wafanya biashara wa Eneo la Fungu refu kudumisha usafi wa mazingira ili kujikinga na Maradhi ya Mripuko. 

    Akizungumza katika Ziara Maalumu ya kutembelea Eneo hilo ili  kuona hali ya usafi wa mazingira ya Eneo hilo, amesema ipo haja ya Wafanya biashara kudumisha usafi wa Eneo lao pamoja na Bishara zao kwani zaidi ya Wagonjwa Kumi na Tano wameripotiwa kutoka Eneo hilo 

SEREKALI KUSIMAMIA UTOAJI ELIMU JUU YA UMILIKI HATI YA MATUMIZI YA ARDHI.

Serekali imesema itahakikisha inasimamia suala la utoaji wa Elimu kwa Wananchi kutambua umuhimu wa kumiliki hati ya matumizi ya Ardhi.

Mh Salha Mohammed Mwinjua Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ameyasema hayo katika hafla ya Uzinduzi wa ugawaji wa hati za haki ya matumizi ya Ardhi kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magaribii amesema umiliki wa hati ya Ardhii unasaidia kupunguza Migogoro ya Ardhi inayojitokeza kwa Wanachi ambao hawajafanya uhakiki katika  maeneo yao. 

SMZ KUENDELEA KUIMARISHA VIWANJA VYA NDEGE

Serikali inafikiria kujenga Jengo la Nne la Abiria ili kurahisisha huduma za usafiri wa Anga Nchini.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Muhamed katika mazungumzo yake na ujumbe wa Watu 9 kutoka Benki ya Exim ya China ukiongozwa Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya usafiri wa Benki ya Exim ya China Chen Zhen, amesema lengo ni kuona wanashirkiana katika masuala ya Miundombinu.

Amesema ujio wa Ujumbe huo pia utatoa fursa ya Ushirikiano katika Miradi ya ujenzi ikiwemo Bandari. 

WAVUVI WADOGO KUJENGEWA UWEZO WA ELIMU YA UVUVI NA BAHARI

Wavuvi wadogo Nchini watanufaika kupitia Mradi wa Uvuvi unaolenga kuwapa Elimu na kubainisha maeneo ambayo wanaweza kuvua pamoja na kuunganishwa na Masoko ya Bidhaa zao.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.