MITI ELFU 14KUPANDWA PWANI YA TUMBE MAGHARIBI WILAYA YA MICHEWENI

MAZINGIRA TUMBE

     Jumla ya Miti Elfu Kumi na Nne (14,000) Aina ya Mikoko imepandwa Shehiya ya Tumbe Magharibi katika Sherehe za kuelekea Maazimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

   Akizungumza Katika Maazimisho hayo , Mkuu wa Wilaya ya Micheweni , Mgeni Khatib Yahya, amesema Serikali inaunga Mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Washirika wa Maendeleo Koica kwa kushirikiana na Wananchi katika Upandaji wa Miti kwa lengo la kuhifadhi Mazingira ,kujikinga na mabadiliko ya Tabia Nchi.

   Mapema Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Koica Tanzania, Manshik Shin, amesema kwa kuzingatia Nafasi ya uhifadhi wa mazingira Koica kwa kushirikiana na Koat, imeamua kuazimisha Siku ya Mazingira kwa kupanda Miti aina ya Mikoko ,ili kusapoti Kilimo cha Mwani pamoja kueka Mazalio Rafiki ya Viumbe wa Baharini.

    Afisa Mdhamin Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Dkt.Salim Moh’d Hamza, amewataka Wanajumuiya kwa kushirikiana na Jamii kuendelea kuitunza Miti hiyo, ili iweze kuishi na kuleta haiba ya mazingira na  rasilimali za Baharini kwa Faida ya Taifa.

    Katika Maadhimisho hayo pia Wananchi walifundishwa namna ya uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

    Siku ya Mazingira huazimishwa Duniani kote kila ifikapo Tarehe 05/Juni ya kila Mwaka, ambapo Kauli Mbiu ni Urejeshwaji wa Ardhi na ustahamilivu wa hali  ya Jangwa na Ukame.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.