Habari

SERIKALI YAZINGATIA SHERIA KATIKA UTAFUTAJI NA UCHUKUAJI WA MIKOPO

        Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo Amesema Serikali inazingatia sheria  za Nchi katika utafutaji na uchukuaji wa Mikopo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya Uwekezaji wakati wa Ziara ya Raisi Dr. Samia Nchini Jamhuri ya KoreaProfesa Kitila Mkumbo amesema Mikopo ni Moja ya Nyenzo muhimu ya kupata mtaji wa kusaidia utekelezaji wa Miradi ya Maendeeleo na uendelezaji wa Sekta za Uzalishaji.

JKU KUZINDUA UVUNAJI WA ZAO LA MPUNGA

   Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar  Kanali Makame  Abdalla Daima  Amewapongeza Maafisa na Wapiganaji wa JKU kwa juhudi kubwa wanazozichukua katika kukuza uzalishaji wa Zao la Mpunga

   Akizindua Uvunaji wa Zao hilo katika Bonde la Kambi ya JKU Upenja Wilaya Kasikazini ‘b’ amesema  Majukumu Makuu ya JKU ni udhalishaji mali pamoja na Malezi ya Vijana ya Ujenzi wa Taifa ambao hufunzwa stadi mbalimbali za kazi kwa lengo la kuweza kujiajiri Wenyewe

KUKUMBUKWA KWA HISTORIA YA UTUMWA KUTASAIDIA KUEPUSHA BIASHARA HIYO ISIJIREJEE NCHINI

   Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema lengo la kuiadhimisha Siku ya Kitaifa ya Kusitishwa kwa Biashara ya Utumwa ni kukumbushia madhara yake ili kuepusha Historia isiweze kujirejea Nchini.

  Waziri Soraga Akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la kuadhimisha Siku hiyo ya Juni 6 1873, Amesema licha ya maazimio mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa kupinga Utumwa, ikiwemo Azimio Nambari 317 (6) la Mwaka 1949, bado kumekuwa na Utumwa Mambo Leo ambao umekuwa ukiendelea katika Sehemu mbali mbali Duniani. 

MH.HEMED AMNADI MGOMBE UBUNGE JIMBO LA KWAHANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

     Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kitaendelea kutekeleza vyema ilani ya Chama kwa kuimarisha Miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini.

    Mjumbe wa Kamati Kuu CCM ambae pia ni Makamo wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah akizungumza katika Ufungaji wa Kampeni za Jimbo la Kwahani pamoja na Kumnadi Mgombea wa Jimbo hilo kwa Tiketi ya CCM amesema Viongozi wamekuwa wakichukua juhudi za kuimarisha Sekta muhimu za Kijamii ikiwemo kuimarisha Sekta ya Afya, Elimu Maji safi na salama na miundombinu rafiki ya ukuaji wa kiuchumi Nchini.

ZECO KUTAFUTA NJIA MBADALA UNAPOKATIKA UMEME

Wajumbe wa Baraza la Wawakili wameliomba Shirika la Umeme Zanzibar ZECO kuchukua hatua za ziada kwa kutafuta njia Mbadala linapotokea tatizo la kukatika kwa huduma ya Umeme

Wakichangia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji Nishati na Madini Wajumbe hao wamesema juhudi zaidi zinahitajika katika kutafuta mbinu nyingine za Nishati Mbadala  ili kusaidia wakati wa kukatika umeme Ghafla

WIZARA YA UTALII NA MAMBO YA KALE INATARAJIA KUFANYA MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI.

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale inatarajia kufanya maonyesho ya Utalii na Uwekezaji katika Viwanja Dimani ili kuiinua Zanzibar Kiuchumi kupitia sekta ya Utalii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Mudrik Ramadhan Soraga  amesema  kukuza uwekezaji katika Visiwa vya Unguja na Pemba ni kutoa fursa kwa wadau wa utalii  na kujiongezea kipato.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WAMETAKIWA AKUZINGATIA KANUNI NA SHERIA

Wasimamizi na Wakuu wa Vituo vya Uchaguzi, wametakiwa kusimamia Wajibu wao katika upigaji Kura wa Ubunge Jimbo la Kwahani linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo.

Akifungua Mafunzo ya Siku Mbili kwa wasimamizi hao, mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Zakia Muhammad Abubakari, amesema ni vyema wakazingatia maelekezo waliyopewa na Tume ya uchaguzi ili kuondosha malalamiko.

Aidha dkt. Zakia amewataka wasimamizi kujiamani na kuzingatia Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wote wa upigaji Kura.

WATENDAJI WA TAKWIMU KWENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOGIA .

Miundombinu ya kisasa ya matumizi ya Teknolojia  ni msingi muhimu wa kuimarisha Ufanisi wa shughuli za Kitakwimu kwa njia ya usahihi  na uwezo wa kuchambua data kwa haraka na kutoa Taarifa zenye ubora wa hali ya juu.

WAAJIRI SEKTA BINAFSI WAMEKUMBUSHWA KUWASILISHA KWA USAHIHI MICHANGO ZSSF

Taasisi za Sekta Binafsi zimekumbushwa kuwasilisha kwa wakati na usahihi michango ya waajiriwa wao katika Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ili kutimiza lengo la kuwawezesha kuwa na hifadhi endelevu ya maisha yao.

JAMII IMETAKIWA KUTOWATENGA WAGONJWA WA SIKOSEL

   Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Maradhi ya Sikocell imeitaka Jamii kutowatenga Watu Wanaoishi na Maradhi hayo kwani ni sawa na mengine.

    Akizungumza kwa Nyakati tofauti katika kutoa elimu kwa  Ugonjwa wa Sikocell kwa Wanafunzi na Walimu wa Skuli ya Dr.Ali Muhammed Shein na Haile Salasi Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu  kutoka Hospital ya Mnazi Moja Dkt.Thuwein Nasor Said amesema hali hiyo itaongeza mapenzi baina yao.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.