SERIKALI YAZINGATIA SHERIA KATIKA UTAFUTAJI NA UCHUKUAJI WA MIKOPO

WAZIRI KITILA MKUMBO

        Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo Amesema Serikali inazingatia sheria  za Nchi katika utafutaji na uchukuaji wa Mikopo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya Uwekezaji wakati wa Ziara ya Raisi Dr. Samia Nchini Jamhuri ya KoreaProfesa Kitila Mkumbo amesema Mikopo ni Moja ya Nyenzo muhimu ya kupata mtaji wa kusaidia utekelezaji wa Miradi ya Maendeeleo na uendelezaji wa Sekta za Uzalishaji.

   Ameyataja Maeneo ya Kipaumbele waliokubaliana Kushirikiana na Jamhuri ya Korea kuwa ni Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo ili kuongeza uzalishaji, utafiti katika Sekta ya Madini, na kukuza Biashara.

   Waziri wa Viwanda na Biashara Dr.Ashatu Kijaji amesema Kiwango cha Biashara kinachofanyika kati ya Nchi zote za Bara la Afrika na Korea ni Asilimia 1 pekee, hali inayo sababishwa na kutofikiwa kwa Viwango vya ubora vya Dunia pamoja na kukosa uendelevu wa biashara.

   Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni ni moja ya Matunda ya Ziara ya Dr.Samia Nchini Korea ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango SMZ Dk.Saada Mkuya Salum alishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Mkopo Nafuu wa Dola Milioni 163.6 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo na hapa anaeleza sababu zilizokwamisha utekelezaji wake kwa muda mrefu.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye ni miongoni mwa Viongozi walioambatana na Raisi samia katika Ziara yake Nchini Korea

  Awali Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus alieleza umuhimu wa Ziara ya Rais Dr.Samia Nchini Korea kwa Taifa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.