KUKUMBUKWA KWA HISTORIA YA UTUMWA KUTASAIDIA KUEPUSHA BIASHARA HIYO ISIJIREJEE NCHINI

WAZIRI SORAGA

   Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema lengo la kuiadhimisha Siku ya Kitaifa ya Kusitishwa kwa Biashara ya Utumwa ni kukumbushia madhara yake ili kuepusha Historia isiweze kujirejea Nchini.

  Waziri Soraga Akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la kuadhimisha Siku hiyo ya Juni 6 1873, Amesema licha ya maazimio mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa kupinga Utumwa, ikiwemo Azimio Nambari 317 (6) la Mwaka 1949, bado kumekuwa na Utumwa Mambo Leo ambao umekuwa ukiendelea katika Sehemu mbali mbali Duniani. 

  Askofu wa Kanisa la Anglikana Elias Chakupewa Amesema Kanisa hilo linalichukuwa suala la kuadhimisha kusitishwa kwa Biashara ya Utumwa kwa umuhimu mkubwa kwasababu lilipo Kanisa hilo ndipo palipokuwa Soko Kuu la Utumwa kabla ya biashara hiyo kuwa haramu.

   Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Aboud Suleiman Jumbe amesema jambo hilo likiendelezwa kwa moyo wa upatanishi, maelewano na Maridhiano litasaidia zaidi kuondoa unyanyapaa na kujenga heshima ya kuwa ni Miongoni mwa Nchi inayosimamia kuadhimisha kukemea na kutojirejea Biashara ya kuuzwa kwa Binaadamu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.