Wasimamizi na Wakuu wa Vituo vya Uchaguzi, wametakiwa kusimamia Wajibu wao katika upigaji Kura wa Ubunge Jimbo la Kwahani linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo.
Akifungua Mafunzo ya Siku Mbili kwa wasimamizi hao, mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Zakia Muhammad Abubakari, amesema ni vyema wakazingatia maelekezo waliyopewa na Tume ya uchaguzi ili kuondosha malalamiko.
Aidha dkt. Zakia amewataka wasimamizi kujiamani na kuzingatia Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wote wa upigaji Kura.
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kwahani Safia Iddi Muhammad, amesema Tume haitomvumilia msimamizi yeyote atakae kwenda kinyume na matakwa ya kazi hiyo.
stories
standard