Katika kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ameshiriki zoezi la upandaji wa miti katika shule ya Msingi Chumbi 'A' Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Zoezi hilo ni sehemu ya hatua ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kutunza mazingira kwa kupandamiti, ambapo upandaji huo wa miti ni sehemu ya upadaji miti mil.13 na laki 5 katika Halmashauri tisa zinazounganisha wilaya saba za mkoa wa Pwani.

Halmashauri zote za Mkoa wa pwani tunaenda kupanda miti milioni 13.5 ambapo kila halmashauri itatakiwa kupanda miti milioni 1.5 baada ya zoezi hilo tunaenda kuzindua ugawaji wa miche mili 1.5 ya mikorosho nayo itaanza kupandwa leo na zoezi hilo litaendelea. La muhimu ni kwamba tumepanda miti kinachofuata ni kuitunza na ni kumbukumbu nzuri, hata tukiona miti hii tunakumbuka kwamba imepandwa katika kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wetu" Alisema RC Kunenge.
Zoezi hilo la upandaji wa miti lilienda sambamba na zoezi la uzinduzi ugawaji wa Miche ya miti ya Korosho mil 1.5, kwa wakulima wa wilaya ya Rufiji katika kwa lengo la kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja wilayani humo kupitia Sekta ya Kilimo. Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Nchini CPA.Reuben Putaputa Putaputa amesema bodi ya korosho imejiwekea Mkakati katika mikoa minne hapa nchini, yaani mkoa wa Pwani, Lindi, Mtwara na Mkoa wa Ruvuma ajitaja kipaumbele ikiwa ni ufufuaji wa Mashamba poli.

