Habari

SEREKALI KUSHIRIKIANA NA MATAIFA MBALI MBALI ILI KUKUZA SEKTA YA UTALII.

Serekali imesema itaendlea kushirikiana na Mataifa mbalimbli ili kuona Sekta ya Utalii inaleta tija kwa Maendeleo ya Wazanzibari .

Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Mh Mudrik Ramadhan Suraga akizungumza na Ugeni wa Balozi wa heshima kutoka Jamica amesema Sekta ya Utalii inaendlea kuimarisha Utalii ili kuona wanapata Washirika watakaoleta maendleo katika Sekta ya Utalii 

TAASISI YA DIRECT AID IMEJIPANGA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA NCHINI

    Kuwepo kwa huduma bora za Afya kutawasaidia Wananchi  kufanya kazi zao kwa ufanisi.

    Hayo yameelezwa na Wakaazi wa Chaani katika Siku ya Matibabu katika Kijiji hicho yalioandaliwa na Taasisi ya Direct Aid Wananchi hao wamesema kuimarika kwa Matibabu ya Kiafya Mwilini kutasaidia kufanya kazi zao kwa wakati hivyo wameishukuru Taasisi hiyo na kukiomba kuwa suala hilo liwe la muendelezo.

WALIMU ZAIDI YA 500 WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO

   Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amalii Mhe.Ali Abdulgulam Hussein amesema kujengewa uwezo Walimu kutasaidia kufikia malengo ya Serikali katika kuimarisha elimu Nchini.

   Akifunga Mafunzo kwa Walimu na Wasaidizi Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja huko Kituo cha Ubunifu Jangombe Naibu Waziri amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Walimu na kuwapatia Mafunzo Kazini ili kufanyakazi kwa ufanisi.

SHIRIKA LA NYUMBA LATAKIWA KUZIFANYIA MATENGENEZO NYUMBA ZINAZOMILKIWA NA SERIKALI

   Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Bi.Khadija Khamis Rajabu amelitaka Shirika la Nyumba kuweka usimamaizi mzuri wa Nyumba  za Serikali  kwa  kuhakikisha wanazifanyia matengenezo na Wananchi  wanalipa  kodi kwa wakati   ili Nyumba hizo ziweze kuleta tija  kwa Serikali . 

FULL SHANGWE MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT)

   Katibu Mkuu Umoja Wanawake Tanzania UWT Taifa Suzan Peter kunambi amewataka Viongozi wa Umoja huo kufanya kazi kwa kutambua kuwa UWT ni Taasisi imara ya kuwasaidia Viongozi wa Nchi katika hatua mbali za Maendeleo

    Akizungumza baada ya Mapokezi na Utambulisho maalum kufuatia kuteuliwa kutumikia nafasi hiyo huko Kisiwandui amesema utulivu wa Viongozi Wakuu wa Nchi unatokana na utendaji wa kazi za Jumuiya hiyo katika njia mbalimbali

WAZIRI TABIA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

     Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya umekuwa ni tatizo nchini na duniani kwa ujumla.

     Ameyasema hayo katika bonanza la kuelekea maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya lililofanyika katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

WATENDAJI WA SERIKALI NCHINI WATAKIWA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

      Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaagiza watendaji wa Serikali nchini kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

     Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Katome, Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Dkt. Biteko amesema ni wajibu wa watendaji wa Serikali kuhakikisha kero za wananchi zinapata ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapatia wananchi maendeleo.

CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA KWAHANI

    Khamis Yussuf Mussa ashinda Uchaguzi wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kwahani, akiwaacha kwa utofauti mkubwa Wagombea wenza katika nafasi hio

Kura zilizopigwa: 7383
Zilizokataliwa: 139
Kura halali: 7333
Wapigaji kura: 10936

     Na baada ya matokeo hayo Mwenyekiti amemtangaza Mgombea kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ameshinda Uchaguzi huo kwa kishindo na amepata kura 7092.

SMT KUANZA KUTOA HUDUMA ZA MAGONJWA YASIOAMBUKIZA KISARAWE

   Serikali inatarajia kuanza kutoa huduma za Kibingwa za Magonjwa yasioambukiza katika Vituo vya Afya ili kuwafikia Wananchi hasa Wanaoishi Maeneo ya Vijijini.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUDUMISHA USAFI ILI KUINGA JAMII NA MARADHI MBALIMBALI

    Baraza la Manispaa Magharibi ‘a’ limewasisitiza Wafanyabiashara  kudumisha usafi katika sehemu zao za Biashara ili kuepukana na Magonjwa ikiwemo KipinduPindu.

    Akizungumza mara baada ya kazi ya Usafi wa mazingira na utoaji wa elimu kwa Wananchi hao huko Kwanyanya Mkurugenzi wa Baraza hilo Said Hasoun Amesema Baraza la Manispaa halitomfumbia macho Mtu yoyote atakaeshindwa kudumisha Usafi na kufuata miongozo ya Kiafya iliyopo Kisheria.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.