Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Bi.Khadija Khamis Rajabu amelitaka Shirika la Nyumba kuweka usimamaizi mzuri wa Nyumba za Serikali kwa kuhakikisha wanazifanyia matengenezo na Wananchi wanalipa kodi kwa wakati ili Nyumba hizo ziweze kuleta tija kwa Serikali .
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo huko Mkoani mara bada ya Ziara yake ya kutembelea na kukagua Nyumba za Serikali huko Madungu , Machomane na Tibirinzi na kusema kuwa kuna changamoto kubwa iliyopo ni Wananchi kutokuwa tayari kulipa Kodi na kupelekea Serikali kukosa Mapato angalau ya kuzifanyia matengenezo madogomadogo Nyumba hizo
Amesema ipo haja kwa Shirika hilo kujipanga ili kuzifanyia matengenezo Nyumba hizo na nyengine kuzijenga upaya ili Wananchi Waishi katika mazingira bora na ulipaji kodi wa nyumba hizo uwe unaendana na uhalisia wa Nyumba ambazo wamepewa
Nae Mkurugenzi Shirika la Nyumba Mwananisha Ali amesema Serikali imejenga Nyumba hizo kwa ajili ya kumsaidia Mwananchi wa Kipato cha Chini kupata Makaazi lakini baadhi ya Wapangaji wamekuwa wakitumia vitisho na lugha chafu wakati wanapotakiwa kulipia Nyumba hizo .
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Shirika la Nyumba Pemba Ndg.Ali Mohd Khamis amekiri kuwa baadhi ya nyumba hizo zimekuwa ni chakavu , na Shrika tayari limeanza kuzifanyia matengenezo..
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ametembelea na kukagua Maeneo ya Viwanja huko Pujini , Mkanyageni na Chokaani ambayo yanatarajiwa kujengwa Nyumba za Bei Nafuu.