SHIRIKA LA NYUMBA LATAKIWA KUZIFANYIA MATENGENEZO NYUMBA ZINAZOMILKIWA NA SERIKALI

NYUMABA ZA MAENDELEO PEMBA

   Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Bi.Khadija Khamis Rajabu amelitaka Shirika la Nyumba kuweka usimamaizi mzuri wa Nyumba  za Serikali  kwa  kuhakikisha wanazifanyia matengenezo na Wananchi  wanalipa  kodi kwa wakati   ili Nyumba hizo ziweze kuleta tija  kwa Serikali . 

   Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo  huko Mkoani  mara bada ya Ziara yake ya  kutembelea na kukagua  Nyumba za  Serikali huko Madungu , Machomane  na Tibirinzi  na  kusema kuwa kuna  changamoto kubwa iliyopo ni Wananchi  kutokuwa tayari kulipa  Kodi na kupelekea Serikali  kukosa Mapato  angalau ya kuzifanyia matengenezo madogomadogo Nyumba hizo 

    Amesema ipo haja  kwa Shirika hilo  kujipanga ili kuzifanyia matengenezo Nyumba hizo na nyengine kuzijenga upaya  ili Wananchi Waishi katika mazingira bora  na ulipaji kodi wa nyumba hizo  uwe unaendana na  uhalisia  wa Nyumba ambazo  wamepewa 

   Nae Mkurugenzi Shirika la Nyumba  Mwananisha Ali  amesema Serikali imejenga Nyumba hizo  kwa ajili ya kumsaidia Mwananchi wa Kipato cha Chini kupata Makaazi lakini baadhi ya Wapangaji wamekuwa wakitumia vitisho na lugha chafu  wakati wanapotakiwa kulipia Nyumba hizo .

   Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi  Shirika la Nyumba Pemba Ndg.Ali Mohd Khamis amekiri kuwa baadhi ya nyumba hizo   zimekuwa ni chakavu , na Shrika tayari limeanza  kuzifanyia matengenezo..

    Katika Ziara hiyo  Katibu Mkuu  huyo ametembelea na kukagua  Maeneo ya Viwanja huko Pujini ,  Mkanyageni na Chokaani ambayo  yanatarajiwa kujengwa Nyumba za Bei Nafuu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.