Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limewathibitisha Wabunge Deo Mnyika, Cecilia Pareso na Nagma Murtaza Giga kuwa Wenyeviti wa Bunge hilo .
Hayo yamejiri baada ya Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu kuwahoji Wabunge kikanuni kama waanafiki Wabunge hao kuwa Wenyeviti wa Bunge.
Wabunge hao waliteuliwa na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan January 25 Mwaka huu Mjini Zanzibar.
Ahadi za Wenyeviti hao ni kuliunganisha Bunge bila kujali itikadi za Vyama vyao. Cecilia Pareso ni Mbunge wa Viti maalum, Mhe Deodatus Mwanyika ni Mbunge wa Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Kilimo na Mifugo na Nagma Murtaza Giga ni Mbunge wa Viti Maalum ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.
Katika hatua nyengine hekaheka za Bungeni zikaendelea wakati wa kuijadili hoja za Serikali, licha ya kukiri hatua kubwa ya maendeleo inayofanywa na Serikali waheshimiwa Wabunge wameitaka Serikali kuwa na
mipango ya muda mrefu ya kutatua kero za Jamii katika nyanja zote za Kijamii.




