Habari

SMZ KUZIGEUZA TAKA KUWA MALI GHAFI ITAKAYOTUMIKA TENA.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya Zanzibar ina Mpango wa kuzigeuza Taka kuwa MAli ghafi inayoweza kutumika tena ikiwemo kutengeneza Mbolea.

Akijibu suali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohamed amesema Wizara kupitia Halmashauri na Mabaraza ya Miji, zimekuwa zikitoa Mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kuweza kuzisarifu Taka hizo.

WAFANYABIASHARA WAWEKEZE KATIKA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA

Wizara ya Maji Nishati na Madini ikishirikiana na Shirika la USAID imeandaa mikakati maalum ya matumizi ya Nishati mbadala hasa Umeme wa Jua, kwa Watumiaji wakiwemo Wawkezaji wa Hoteli Nchini.

Huyo ni Said Omar Abdalla, Mkuu wa Divisheni ya maendeleo ya Nishati kutoka idara ya Nishati na Madini Zanzibar akimuakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Said Hadi Mdungi amesema kuwepo kwa matumizi ya Nishati hiyo kutaondoa matatizo ya Umeme mdogo, hasa kwa Wafanyabiashara hao wenye mahitaji makubwa zaidi katika sguhuli zao.

BODI MPYA YA MIKOPO IMETAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA UADILIFU UTOAJI WA MIKOPO

    Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali Mhe Ali Abdulgulam Hussein amewahimiza Wajumbe wa Bodi ya Usimamizi wa Mikopo ya Elimu juu kusimamia haki na uadilifu kwa kuhakikisha Mikopo inatolewa kwa walengwa.

RAIS MWINYI ATEMBELEA CHUO CHA UFUNDI CHA AL MUBARAK MAZRUI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekitembelea Chuo cha Ufundi cha Al-Mubarak Mazrui cha Taasisi ya Al-Mazrui Charitable Oganization ya Abu Dhabi, kilichopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi 

   Katika Ziara yake Kituoni hapo Rais Dk.Mwinyi amewataka Wanafunzi wanaopata Mafunzo ya ufundi Kituoni hapo kuendeleza jitihada na kujifunza kwa bidii.

MFUKO WA TIMIZA WATOA FURSA KWA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI

   Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Raisi, Fedha na Mipango Dk.Sada Mkuya Salum amesema kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa pamoja wa Timiza kutasaidia kutoa fursa kwa Wananchi hasa wa kipato cha chini kushiriki katika Uwekezaji na shughuli za kukuza Uchumi.

    Akizungumza katika Uzinduzi wa Mfuko huo kwa niaba ya Dk. Sada Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juma Makungu Juma amesema malengo ya mfuko wa Timiza ni kutoa nafasi zaidi kwa Wananchi kuwekeza na kunufaika kupitia mfuko wa Soko la Fedha.

WASHIRIKI KONGAMANO MIAKA 60 YA MAPINDUZI WATOA MAONI UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO.

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka Washiriki wa Kongamano la Miaka 60 ya Mapinduzi kulitumia Kongamano hilo kujadili na kutoa maoni kwa Serikali kuhusiana na fursa zilizopo katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

    Akifungua Kongamano la  Miaka 60 ya kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein Dkt.Mwinyi amesema ni vyema kuhusisha sera na mpango mkuu wa Serikali kupitia vipaumbele vilivyowekwa.

WIZARA YA NCHI AFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO IMEPANGA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI

Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango imepanga kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kutekeleza Bajeti yenye kuzingatia upembuzi yakinifu kuhusu uanzishaji wa Soko la Hisa pamoja na Benki ya uwekezaji Zanzibar .

Akiwasilisha hutuba ya makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka 2024/2025 Waziri wa Wizra hiyo Saada Mkuya Salum amesema Mpango huo unakusudia pia kuimarisha utoaji wa huduma kwa Wafanyabiashara Wadogo pamoja na ukusanyaji wa mapato katika Masoko mapya

TUME YA UTUMISHI IDARA MAALUM ZA SMZ JIEPUSHENI NA MIVUTANO

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, ameitaka tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ, kuhaki    kisha matatizo ya kiutumishi yanapatiwa ufumbuzi.

Akizungumza Afisini kwake Vuga na wajumbe wa tume hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni, ameitaka  kuwa daraja la kuwaunganisha askari kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia Idara Maalum za SMZ.

WATENDAJI WA MANISPAA MJINI KUBUNI MIKAKATI KUIMARISHA USAFI.

Watendaji wa baraza la manispaa mjini wametakiwa  kubuni mpango mkakati ya miongozo ya kiutendaji kwa lengo la kuimarisha hali ya usafi wa mazingira ya mji wa zanzibar.

Akizindua   vikapu vya kuhifadhia taka  huko maruhubi   kwa niaba ya waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mkuu wa mkoa wa mjini magharibi idrisa kitwana mustafa   amesema  hatua hiyo itasaidia kukuza  taaluma za uvumbuzi na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

SHERIA BORA YA HABARI KUIMARISHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO imeadhimia kufuatilia kwa karibu zaidi Sheria mpya za habari ambazo Zina mapungufu yanayoathiri ukusanyaji na upokeaji habari

Akizungumza katika tathimini ya maadhimisho ya Siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC Abdallah Mfaume amesema kuendelea kuwepo Sheria zisizo sahihi ni kuzorotesha kasi ya usatawi wa Demokrasia

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.