MFUKO WA TIMIZA WATOA FURSA KWA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI

NAIBU WAZIRI FEDHA

   Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Raisi, Fedha na Mipango Dk.Sada Mkuya Salum amesema kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa pamoja wa Timiza kutasaidia kutoa fursa kwa Wananchi hasa wa kipato cha chini kushiriki katika Uwekezaji na shughuli za kukuza Uchumi.

    Akizungumza katika Uzinduzi wa Mfuko huo kwa niaba ya Dk. Sada Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juma Makungu Juma amesema malengo ya mfuko wa Timiza ni kutoa nafasi zaidi kwa Wananchi kuwekeza na kunufaika kupitia mfuko wa Soko la Fedha.

   Wakielezea umuhimu na mchango wa mfuko wa Timiza Watendaji kutoka Taasisi tofauti za Tanzania Bara na Zanzibar  wamesema Mfuko huo utawezesha kuinuwa Kipato cha Wawekezaji Wadogo, wakati na wakubwa pamoja na kuongeza kasi ya ukuwaji wa Uchumi wa Nchi.

    Timiza ni Mfuko wa Uwekezaji unaomuwezesha Mwananchi kuwekeza kuanzia Shilingi elfu 10 ambao umeanzishwa na Kampuni  ya Zan Securities kwa lengo la kuwashirikisha Wananchi kujiunga na mfumo wa Soko la mitaji na dhamana ili kunufaika Kiuchumi. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.