Watendaji wa baraza la manispaa mjini wametakiwa kubuni mpango mkakati ya miongozo ya kiutendaji kwa lengo la kuimarisha hali ya usafi wa mazingira ya mji wa zanzibar.
Akizindua vikapu vya kuhifadhia taka huko maruhubi kwa niaba ya waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mkuu wa mkoa wa mjini magharibi idrisa kitwana mustafa amesema hatua hiyo itasaidia kukuza taaluma za uvumbuzi na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Naibu mstahiki mea wa jiji la zanzibar khadija ame haji na mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini ali khamis muhammed wamesema uchakavu na upungufu wa vifaa kusababisha manispaa ya mjini kuwa na mrundiko mkubwa wa taka .
Watendaji wa manispaa hiyo wamesema watashirikiana pamoja kuhakikisha wanasimamia majukumu yao ya kazi na pamoja na kuiomba jamii kuzihifadhi taka kwa kuziweka katika viakapu hivyo ili kuepusha kuzagaa ovyo.