Habari

RC LINDI AZITAKA HALMASHAURI ZA MKOANI HUMO KUUNDA MADAWATI YA ULINZI YA WATOTO PAMOJA NA KLABU ZA WATOTO MASHULENI

    Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha zinafufua au kuunda madawati ya ulinzi ya watoto  sambamba na kuunda klabu za watoto mashuleni zitakazowasaidia kuelezea na kutatua changamoto zao

RAIS DKT.MWINYI AZINDUA KIGODA CHA TAALUMA CHA SHEIKH ABEID AMANI KARUME

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekitaka Kigoda cha taaluma cha Sheikh Abeid Amani Karume kutilia mkazo zaidi masuala ya kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya maendeleo nchini.

     Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozindua rasmi Kigoda cha taaluma cha Sheikh Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 15 Juni 2024.

SHIRIKISHO LA MACHINGA RUKWA YAFANYA KONGAMANO

     Kongamano la Shirikisho la  Machinga Tanzania limefanyika Mkoani Rukwa kwa  kumpongeza Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga Kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 18.5 kwa ajili ya kuwakopesha Wajasiriamali(Machinga) Nchi nzima.

BEI ZA BIDHAA ZASHUKA KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU

   Kuelekea msimu huu wa Idil-Adhhaa baadhi ya Bidhaa zimeonekana kushuka Bei ukilinganisha na Sikukuu ya Eid _Fitri.

   Hayo yamejiri baada ya ZBC kuzungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe C ambapo wamesema upatikanaji wa bidhaa umekuwa mkubwa msimu huu na kupelekea kushuka kwa Bei za bidhaa kama vile Mchele, Tungule, Nyama, Mafuta , Vitunguu na nyinginezo jambo ambalo linaleta unafuu wa  maisha katika Kipindi cha Sikukuu.

ZANZIBAR YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MAJANGA YA DHARURA

     Serikali imekuwa ikichukuwa juhudi za kukabiliana na dharura za Kiafya ili kuhakikisha Nchi inaendelea kubaki salama dhidi ya Majanga mbalimbali ikiwemo Magonjwa ya Miripuko

    Akifungua Mkutano wa Kitaalamu  wa Dunia ,juu ya Mipango Miji na kuweka Mikakati ya Majanga ya dharura  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Dk Islam Seif Amesema ili juhudi hizo ziweze kufanya kazi Wananchi nao wana wajibu mkubwa wa kufikiria namna ya kuimarisha mazingira 

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YATAONGEZA KASI YA UDHIBITI BIASHARA HARAMU

     Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohammed amesema mafunzo ya kupambana na kuthidibiti dawa za kulevya yataongeza kasi ya kudhibiti biashara hiyo haramu.

    Akifunga mafunzo ya siku moja ya kamati za ulinzi na usalama za Mikoa ya Unguja, huko ukumbi wa Shirika la Bima Zanzibar, amesema anaimani kuwa mafunzo yaliyotolewa yatumike kuunganisha nguvu dhidi ya mapambano na uhalifu wa dawa za kulevya kwa maslahi ya kizazi cha baadae na Taifa kwa ujumla.

ZHC WAMEFANIKIWA KUUZA NYUMBA 72 ZENYE THAMANI YA BILIONI 5.5

      Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mhe Dkt.Saada Mkuya Salum katika Baraza la Wawakilishi ametoa ufafanunuzi wa bajeti katika Sekta mbalimbali za Serikali.

      “Baraza la Wawakilishi liliridhia mapendekezo ya Serikali kwa kutoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa Miradi ya Nyumba Nafuu (Affordable Housing Scheme) ili kuimarisha makaazi bora kwa wananchi pamoja na kupunguza gharama za ununuzi wa nyumba hizo”

BAJETI KUU KUZINGATIA UIMARISHAJI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI

    Hali ya Uchumi wa Zanzibar inakadiriwa kukuwa kwa Mwaka 2024 kwa wastani wa Asilimia 7 nukta 2 kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ongezeko la uingiaji watalii wanaoitembelea Zanzibar kwa Asilimia 30 pamoja na utekelezaji wa Miradi mikubwa ya kimkakati 

DK MWINYI AMEWATAKA WAMILIKI WA HOTELI ZA KITALII KUNUNUA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA WANANCHI.

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi ameiagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais kazi uchumi na uwekezaji kuhakikisha wamiliki wa Hoteli za kitalii wananunua bidhaa zinazozalishwa na Wananchi.

Akizungumza katika Ufunguzi wa mradi wa hoteli ya The mora Zanzibar Kijiji cha Matemwe Dk Mwinyi amesema hiyo ni miongoni mwa Mipango ya Serikali kuhakikisha uwekezaji unanufaisha pande zote ikiwemo wawekezaji, Wananchi na Serikali.

HUDUMA ZA KIJAMII KUWEPO KATIKA MAENEO YA MIJI MIPYA

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Mudriq Ramadhan Soraga amesema huduma za Msingi za Kijamii ni muhimu ziwepo katika maeneo ya Miji mipya kwani Serikali inaendelea kutoa msisitizo kwa wawekezaji kuweka huduma za Kimtandao katika maeneo hayo.

Akizungumza na Wadau wa uwekezaji wa Ujenzi wa Miji Mipya na Maendeleo ya Kiuchumi Zanzibar huko Fumba Town amesema Sekta ya Ujenzi ya Nyumba za Makazi inakuwa kwa haraka kwani imetoa Vivutio vikubwa ambapo Wawekezaji wanajitokeza.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.