MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YATAONGEZA KASI YA UDHIBITI BIASHARA HARAMU

Waziri Masoud

     Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohammed amesema mafunzo ya kupambana na kuthidibiti dawa za kulevya yataongeza kasi ya kudhibiti biashara hiyo haramu.

    Akifunga mafunzo ya siku moja ya kamati za ulinzi na usalama za Mikoa ya Unguja, huko ukumbi wa Shirika la Bima Zanzibar, amesema anaimani kuwa mafunzo yaliyotolewa yatumike kuunganisha nguvu dhidi ya mapambano na uhalifu wa dawa za kulevya kwa maslahi ya kizazi cha baadae na Taifa kwa ujumla.

    Aidha, Waziri Masoud amesema mafanikio ya kudhibiti uhalifu wa dawa za kulevya yatafikiwa endapo kila moja atatimiza wajibu wake ipasavyo.

     Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghsrib, Idrisa Kitwana Mustafa, amesema hawatosita kumchukulia hatua mtu yoyote anaejihusisha na dawa za kulevya.

    Mafunzo hayo yameandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar ambapo mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni athari ya dawa za kulevya, Sheria za dawa za kulevya na wajibu wa kamati za ulinzi na usalama katika uhalifu wa dawa za kulevya na hatua za kupambana nazo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.