Kuelekea msimu huu wa Idil-Adhhaa baadhi ya Bidhaa zimeonekana kushuka Bei ukilinganisha na Sikukuu ya Eid _Fitri.
Hayo yamejiri baada ya ZBC kuzungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe C ambapo wamesema upatikanaji wa bidhaa umekuwa mkubwa msimu huu na kupelekea kushuka kwa Bei za bidhaa kama vile Mchele, Tungule, Nyama, Mafuta , Vitunguu na nyinginezo jambo ambalo linaleta unafuu wa maisha katika Kipindi cha Sikukuu.
Baadhi ya Wanunuzi wanaofika Sokoni hapo wamesema wanafurahishwa na hali ya hiyo kwani kushuka kwa Bidhaa hizo kutawasaidia kuondokana na adha ya Mfumuko wa Bei kuelekea Msimu wa Sikukuu.
Mkuu wa Soko la Mwanakwerkwe C Sharif Ali Sharif amesema kutokana urahisi wa upatikanaji wa Bidhaa kwa wingi Sokoni hapo amewataka Wafanyabiashara hao kutopandisha Bei kwa kujali Maslahi yao Binafsi.