Habari

UONGOZI WA ZBC WAFANYA ZIARA YA UKAGUZI KATIKA JENGO LA SHIRIKA RAHALEO

    Uongozi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC umefanya Ziara ya Ukaguzi katika Jengo la Shirika hilo Rahaleo ili kuona hatua za matengenezo zinazoendelea  katika Jengo.

     Mkurugenzi wa ZBC Ndg.Ramadhani Bukini, ameelezea kuridhishwa na hatua zinazoendelea za matengenezo hayo ambpo Mwezi huu wa Juni Jengo hilo litakuwa na muonekano mpya.

    fundi Mkuu wa Shirika la ZBC Ndg.Ali Aboud amesema Matengenezo hayo utawezesha TV na Redio kuwa katika Jengo hilo pamoja na ongezeko la Studio za shughuli mbalimbali za Kihabari zitakuwepo .

UTUNZAJI KUMBUKUMBU WA KIELETRONIKI UTASAIDIA KUENDANA NA MABADILIKO YA UCHUMI WA KIDIGITALI AFRIKA

   Taasisi za Umma na Binafsi zinashauriwa kutumia Mfumo wa  Kieletroniki katika utunzaji wa kumbukumbu ili kuendana na mabadiliko ya uchumi wa kidigitali Barani Afrika.

    Akizungumza katika Mkutano wa 41 wa Taasisi ya usimamizi wa kumbukumbu Afrika RMFA Muandaaji wa Mkutano huo unaofanyika Zanzibar kwa mara ya Tatu Grace Donath Kaganga amesema utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kupitia Mfumo wa Kieletroniki unahakikisha usalama zaidi dhidi ya madhara mbalimbali. 

MAMA MARIAM MWINYI AGAWA TAULO ZA KIKE SKULI YA SEKONDARI MICHEWENI

     Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi amesema suala la kumkomboa msichana wa Zanzibar linahitaji ushiriki wa taasisi zote za umma na binafsi pamoja na jamii kwa ujumla wakiwemo wazazi na walezi.

     Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo katika hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Micheweni, kwa ajili ya hedhi salama Mkoa wa Kaskazini Pemba  tarehe.

DKT.SAMIA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUHAMASISHA KUPOKEA UJUZI MPYA TAARIFA ZA MAENDELEO YA KITEKNOLOJIA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii, vifichue maovu na kutowajibika kunakofanywa na Watumishi na Watendaji wa Serikali, vinatoa mrejesho wa hisia na mtazamo wa wananchi kwa Serikali yao, na kwa ujumla, vinafanya kazi ya kuelimisha na kukuza demokrasia.

SMZ INADHAMIRA YA KUANZISHA MFUKO WA HIJJA ZANZIBAR

Serikali   ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inadhamira ya kuanzisha Mfuko wa Hijja Zanzibar ili kuwawezesha wananchi kupatafursa ya kwenda kufanya ibada hiyo Nchini Sudia Rabia.

Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk Hussein Ali Mwinyi  amesema hayo  wakati alipokuwa akizungumza na Waumini wa dini ya kiislamu huko katika Viwanja vya Mabutu Mjini Wingwi katika wilaya ya Micheweni Pemba    katika hafla ya Baraza la  Eid El Adhha lilofanyika Kisiwani humo..

NGOMBE 35 WA SADAKA WAMECHINJWA KATIKA CHINJIO LA KISAKASAKA

Jumuiya  inayojishughulisha na huduma za Jamii Directaid   Zanzibar   imechinja Ng’ombe 35   kwa ajili ya  kutoa sadaka ya Sikukuu ya Eid El -Adhaha  ikiwa ni utaratibu  wa kila ifikapo mfunguo Tatu.

Akizungumza  na ZBC katika machinjio ya kisakasaka Afisa wa Manunuzi  wa Jumuiya hiyo ali Suleiman  Ali amesema Jumuiya hiyo itaendelea  kutoa Sadaka hiyo  maeneo ya Mjini pamoja na  Vijijini ili Jamii    iweze kukidhi mahitaji ya SIkukuu.

WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VISIVO NA MAADILI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kujiepusha na Vitendo vinavyoenda tofauti na Mila na Desturi za Tanzania na kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo Nchini.

Waziri mkuu Majaliwa maetoa Kauli hiyo kwenye Baraza la Eid El Adh’haa Kitaifa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed Vi Makamo Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Jijini Dar es salaam mara baada ya kukamilika kwa swala Sikukuu ya Eid El Adh’haa.

MWENYEKITI CCM MKOA WA MJINI KICHAMA AMEWATAKIA IDDI ADHA WAUMINI WA KIISLAM.

Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali  amesema Mwenyezi Mungu huteremsha Neema kubwa katika Mikusanyiko yenye Kheri na kuwatakia Iddi Adha Waumini wote wa Kiislam

Akitoa Sadaka ya Kuku kwa Viongozi na Wanachama wa CCM katika kusherehekea Sikukuu ya Edd Adh huko Amani  Mkoa.

Amesema kutoa Sadaka kwa Mwenye nacho kunasaidia kwa walokuwa hawana uwezo kufurahi katika kipindi hiki cha furaha.

Nao baadhi ya viongozi waliopata Sadaka hiya wamesifu hatua ya kiongozi wao.

SUALA LA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE LINAHITAJI USHIRIKIANO NA JAMII.

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi amesema suala la kumkomboa Mtoto wa Kike linahitaji Ushirikiano wa Taasisi zote za Umma na Binafsi na  Jamii.

Akizungumza katika Viwanja vya Shamata, Wilaya ya Micheweni, kwenye hafla ya ugawaji wa Taulo za Kike kwa Wanafunzi wa Kike wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni amesema, Mtoto wa Kike ana haki ya kupata Elimu kama Mtoto wa Kiume.

WANANCHI WA SHUMBA MJINI WAMETAKIWA KUZUIA UNGIAJI WA HARAMU WA BINADAMU.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan amewataka Wananchi wa Shumba ya Mjini Kisiwani Pemba,kusimama imara katika kuhakikisha wanazuia ingiaji wa Wageni kinyume na Sheria .

Kamishamna ametoa kauli hiyo wakati akizumza na Wananchi wa Shumba ya Mjini katika ziara yake ya kuskiliaza Changamoto zinazojitokeza Wananchi hao hao.

Amesema katika bandari ya Shumba kumekuwepo  na Ungiaji wa Wageni kinyume na Sheria ambao sio Waaminifu.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.