MAMA MARIAM MWINYI AGAWA TAULO ZA KIKE SKULI YA SEKONDARI MICHEWENI

Mama Mariam Mwinyi

     Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi amesema suala la kumkomboa msichana wa Zanzibar linahitaji ushiriki wa taasisi zote za umma na binafsi pamoja na jamii kwa ujumla wakiwemo wazazi na walezi.

     Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo katika hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Micheweni, kwa ajili ya hedhi salama Mkoa wa Kaskazini Pemba  tarehe.

      Aidha Mama Mariam Mwinyi amesema Wasichana wana haki ya kupata fursa sawa ya elimu kama watoto wa kiume kwani nao ni walezi wa familia na jamii kwa ujumla.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.