NGOMBE 35 WA SADAKA WAMECHINJWA KATIKA CHINJIO LA KISAKASAKA

AFISA NMANUNUZI  DIRECTAID

Jumuiya  inayojishughulisha na huduma za Jamii Directaid   Zanzibar   imechinja Ng’ombe 35   kwa ajili ya  kutoa sadaka ya Sikukuu ya Eid El -Adhaha  ikiwa ni utaratibu  wa kila ifikapo mfunguo Tatu.

Akizungumza  na ZBC katika machinjio ya kisakasaka Afisa wa Manunuzi  wa Jumuiya hiyo ali Suleiman  Ali amesema Jumuiya hiyo itaendelea  kutoa Sadaka hiyo  maeneo ya Mjini pamoja na  Vijijini ili Jamii    iweze kukidhi mahitaji ya SIkukuu.

Daktari wa Mifugo  kutoka Wakala wa Chakula na  Dawa  Thamra Khamis Talib   amewatoa hofu  Watumiaji wa nyama   ya Ng’ombe ambao Wanachinjwa  eneo hilo  la Kisakasaka   na kusema kuwa  wamezingatia ubora baada ya kufanyiwa Uchunguzi

Mwenyekiti wa Wachinjaji  Idrisa Othman Iddi  amesema  kazi ya  Uchinjaji  imekwenda vizuri   pamoja na kukabiliwa na    Tatizo la  Miundombinu  pamoja na uchakavu wa Jengo Wanalofanyia kazi hiyo.

Wananchi  wanaofuata kupata Sadaka     ya Nyama wameomba  kuwekwa kwa utaratibu  maalum  utakaosadia kupuinguza  usumbufu wa kusubiri  kwa  muda mrefu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.