UONGOZI WA ZBC WAFANYA ZIARA YA UKAGUZI KATIKA JENGO LA SHIRIKA RAHALEO

ZBC UKAGUZI

    Uongozi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC umefanya Ziara ya Ukaguzi katika Jengo la Shirika hilo Rahaleo ili kuona hatua za matengenezo zinazoendelea  katika Jengo.

     Mkurugenzi wa ZBC Ndg.Ramadhani Bukini, ameelezea kuridhishwa na hatua zinazoendelea za matengenezo hayo ambpo Mwezi huu wa Juni Jengo hilo litakuwa na muonekano mpya.

    fundi Mkuu wa Shirika la ZBC Ndg.Ali Aboud amesema Matengenezo hayo utawezesha TV na Redio kuwa katika Jengo hilo pamoja na ongezeko la Studio za shughuli mbalimbali za Kihabari zitakuwepo .

   Wakandarasi kutoka China wanaofanya  Matengenezo hayo wameahidi kumaliza Ujenzi huo kwa wakati Mwezi huu ambapo Vifaa vinatarajiwa kuingia  Nchini Muda wowote kuanzia Sasa.

    Matengenezo ya  Jengo la Shirika la Utangazaji Zanzibar ni Ufadhili wa Serikali ya China kwa kushirikiana na SMZ.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.