DKT.SAMIA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUHAMASISHA KUPOKEA UJUZI MPYA TAARIFA ZA MAENDELEO YA KITEKNOLOJIA

Dkt.Samia

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii, vifichue maovu na kutowajibika kunakofanywa na Watumishi na Watendaji wa Serikali, vinatoa mrejesho wa hisia na mtazamo wa wananchi kwa Serikali yao, na kwa ujumla, vinafanya kazi ya kuelimisha na kukuza demokrasia.

     Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa masuala haya ndiyo yanayoifanya Serikali kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na vyombo vya habari.

     Vile vile, Rais Samia amesema Vyombo vya habari sio mshindani wa Serikali bali ni mdau na mshiriki muhimu katika yanayotendwa na Serikali hivyo, Serikali itaendelea kuweka mifumo mizuri ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi, katika kuimarisha uhuru na mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.