SMZ INADHAMIRA YA KUANZISHA MFUKO WA HIJJA ZANZIBAR

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Serikali   ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inadhamira ya kuanzisha Mfuko wa Hijja Zanzibar ili kuwawezesha wananchi kupatafursa ya kwenda kufanya ibada hiyo Nchini Sudia Rabia.

Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk Hussein Ali Mwinyi  amesema hayo  wakati alipokuwa akizungumza na Waumini wa dini ya kiislamu huko katika Viwanja vya Mabutu Mjini Wingwi katika wilaya ya Micheweni Pemba    katika hafla ya Baraza la  Eid El Adhha lilofanyika Kisiwani humo..

Aidha ameipongeza Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana kwa kuwashajihisha Wananchi juu ya umuhimu wa kwenda Hijja kwa kushirikiana na  Taasisi zinazo safirisha Mahujjaj kwa kuratibu safari hizo jambo ambalo limesababisha  ongezeko kubwa la mahujjaj Zanzibar na Tanzania kwa ujumla .

Akizungumza  kuhushu shughu za maendeleo Mh. Rais amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali  katika kuendeleza Miradi hio ikiwemo Ujenzi wa Bara Bara  na Miradi mengine  mengine inayotekelezwa na Serikali.

Amesema  Serikali inaendelea kujenga Bandari ya shumba Mjini Kisiwani Pemba sambamba na Ujenzi wa Skuli za Ghorofa, Nyumba za Walimu na Miradi mengine mbali mbali

Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dr.  Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha Amani na utulivu uliopo kwani ndio inayowapelekea kufanya ibada zao kwa Uhuru na kujiletea maendeleo

Mapema wakati wa asubuhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi alijumuika na Waumini wa Kiislam kutoka Mikoa miwili ya Kisiwani pemba katika sala  ya Eid El Hajj   kufuatia kumalizia kwa ibada ya hijja huko Makkah Mjini Saudi Arabia iliyosaliwa katika viwanja vya Mshaame Mata Micheweni Pemba.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.