Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inadhamira ya kuanzisha Mfuko wa Hijja Zanzibar ili kuwawezesha wananchi kupatafursa ya kwenda kufanya ibada hiyo Nchini Sudia Rabia.
Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk Hussein Ali Mwinyi amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Waumini wa dini ya kiislamu huko katika Viwanja vya Mabutu Mjini Wingwi katika wilaya ya Micheweni Pemba katika hafla ya Baraza la Eid El Adhha lilofanyika Kisiwani humo..
Aidha ameipongeza Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana kwa kuwashajihisha Wananchi juu ya umuhimu wa kwenda Hijja kwa kushirikiana na Taasisi zinazo safirisha Mahujjaj kwa kuratibu safari hizo jambo ambalo limesababisha ongezeko kubwa la mahujjaj Zanzibar na Tanzania kwa ujumla .
Akizungumza kuhushu shughu za maendeleo Mh. Rais amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza Miradi hio ikiwemo Ujenzi wa Bara Bara na Miradi mengine mengine inayotekelezwa na Serikali.
Amesema Serikali inaendelea kujenga Bandari ya shumba Mjini Kisiwani Pemba sambamba na Ujenzi wa Skuli za Ghorofa, Nyumba za Walimu na Miradi mengine mbali mbali
Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dr. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha Amani na utulivu uliopo kwani ndio inayowapelekea kufanya ibada zao kwa Uhuru na kujiletea maendeleo
Mapema wakati wa asubuhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi alijumuika na Waumini wa Kiislam kutoka Mikoa miwili ya Kisiwani pemba katika sala ya Eid El Hajj kufuatia kumalizia kwa ibada ya hijja huko Makkah Mjini Saudi Arabia iliyosaliwa katika viwanja vya Mshaame Mata Micheweni Pemba.