SUALA LA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE LINAHITAJI USHIRIKIANO NA JAMII.

MAMA MARIAM MWINYI

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi amesema suala la kumkomboa Mtoto wa Kike linahitaji Ushirikiano wa Taasisi zote za Umma na Binafsi na  Jamii.

Akizungumza katika Viwanja vya Shamata, Wilaya ya Micheweni, kwenye hafla ya ugawaji wa Taulo za Kike kwa Wanafunzi wa Kike wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni amesema, Mtoto wa Kike ana haki ya kupata Elimu kama Mtoto wa Kiume.

Aidha Mama Mariam ameisifu jitihada zinazochukuliwa na Taasisi ya “Lady Fatma ya Korea ya Kusini kwa kuunga Mkono malengo ya Mradi wa “Tumaini Initiative” kumkomboa Mtoto wa kike kwa kutengeneza vifaa vya kujihifadhi Wanawake.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Ali Abdul Gulam Hussein ameipongeza Taasisi hiyo  kwa jitihada zake za kuisaidia Serikali kupitia ushiriki wake wa kuendelea kuwawaweka salama Watoto wa Kike.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, salama Mbarouk Khatibu amesema, hivi karibuni Taasisi hiyo imewafikia wananchi wa mkoa huo     baada ya kuweka kambi ya matibabu bure ambapo Wananchi zaidi ya Elfu Tisa wamepatiwa matibabu.

Mratibu wa Taasisi ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation”, Gulam Abdul Karim, amesema lengo  la mradi wa “Tumaini Initiative” ni kutatua matatizo ya Watoto wa Kike

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.