Serikali imekuwa ikichukuwa juhudi za kukabiliana na dharura za Kiafya ili kuhakikisha Nchi inaendelea kubaki salama dhidi ya Majanga mbalimbali ikiwemo Magonjwa ya Miripuko
Akifungua Mkutano wa Kitaalamu wa Dunia ,juu ya Mipango Miji na kuweka Mikakati ya Majanga ya dharura Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Dk Islam Seif Amesema ili juhudi hizo ziweze kufanya kazi Wananchi nao wana wajibu mkubwa wa kufikiria namna ya kuimarisha mazingira
Amesema kufanyika Mkutano huo ni heshima kwa Zanzibar hivyo Wananchi waone umuhimu wake kwani ni fursa kwa wengine kujifunza Zanzibar ilivyoweza kukabiliana na Magonjwa ya Miripuko ikiwemo Covid na Kipindupindu
Mwakilishi Shirika la Afya Duniani WHO Zanzibar Dk t.Andemichael Ghirmay amesema ukuwaji wa Miji Barani Afrika umeongezeka kwa Asilimia 64 huku Maeneo hayo yakigeuka kuwa Maeneo ya Uchumi
Hivyo upangaji mbaya wa Miji utasababisha Mailioni ya Watu kukabiliwa na Maafa hapo baadae
Mkutano huo wa Siku Mbili uliowakutanisha Wataalamu wa Dunia wa mipango Miji umeandaliwa na Shirika la Afya Duniani who