ZANZIBAR YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MAJANGA YA DHARURA

MKUTANO WA KITAALUMA DUNIANI

     Serikali imekuwa ikichukuwa juhudi za kukabiliana na dharura za Kiafya ili kuhakikisha Nchi inaendelea kubaki salama dhidi ya Majanga mbalimbali ikiwemo Magonjwa ya Miripuko

    Akifungua Mkutano wa Kitaalamu  wa Dunia ,juu ya Mipango Miji na kuweka Mikakati ya Majanga ya dharura  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Dk Islam Seif Amesema ili juhudi hizo ziweze kufanya kazi Wananchi nao wana wajibu mkubwa wa kufikiria namna ya kuimarisha mazingira 

    Amesema kufanyika Mkutano huo ni heshima kwa Zanzibar hivyo Wananchi waone umuhimu wake kwani ni fursa kwa wengine kujifunza Zanzibar ilivyoweza kukabiliana na Magonjwa ya Miripuko ikiwemo Covid na Kipindupindu 

   Mwakilishi Shirika la Afya Duniani WHO Zanzibar Dk t.Andemichael Ghirmay amesema ukuwaji wa Miji Barani Afrika umeongezeka kwa Asilimia 64 huku Maeneo hayo yakigeuka kuwa Maeneo ya Uchumi 

   Hivyo upangaji mbaya wa Miji utasababisha Mailioni ya Watu kukabiliwa na Maafa hapo baadae

    Mkutano huo wa Siku Mbili uliowakutanisha Wataalamu wa Dunia wa mipango Miji umeandaliwa na Shirika la Afya Duniani who

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.