Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi ameiagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais kazi uchumi na uwekezaji kuhakikisha wamiliki wa Hoteli za kitalii wananunua bidhaa zinazozalishwa na Wananchi.
Akizungumza katika Ufunguzi wa mradi wa hoteli ya The mora Zanzibar Kijiji cha Matemwe Dk Mwinyi amesema hiyo ni miongoni mwa Mipango ya Serikali kuhakikisha uwekezaji unanufaisha pande zote ikiwemo wawekezaji, Wananchi na Serikali.
Amesema ni wajibu wa kila muwekezaji kutambua kuwa ni wajibu wake kuzungumza na Uongozi wa eneo husika analotarajia kuwekeza kusaidia huduma za Kijamii ikiwemo Maji ,Elimu na afya ili kuimarisha mazingira ya wananchi hao
Akizungumzia kuhusiana na mkakati wa kuimarisha mazingira ya uwekezaji Dk Mwinyi amesema karibu asilimia 30 ya Uchumi unatokana na Utalii hivyo wanatarajia kujenga Uwanja wa Ndege Pemba ili kuruhusu kutua Ndege kubwa kuifungua Pemba Kiuchumi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais kazi,Uchumi na uwekezaji Mh Shariff Ali Shariff amesema ufunguzi wa Mradi huo hapa Zanzibar ni kuidhihirishia Dunia kuwa Zanzibar inaendelea kufanya vizuri katika Sekta ya Utalii
Mkurugenzi Mtendaji mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar Zipa Saleh Sadi Mohammed amepongeza Wawekezaji kuendelea kuwekeza Miradi mikubwa ambayo inaongeza Pato la Serikali.
Mradi huo umeogharimu Dola Milioni 500 umetoa ajira zaidi ya Mia Sita kwa vijana wakiwemo Wazalendo