Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, ameitaka tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ, kuhaki kisha matatizo ya kiutumishi yanapatiwa ufumbuzi.
Akizungumza Afisini kwake Vuga na wajumbe wa tume hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni, ameitaka kuwa daraja la kuwaunganisha askari kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia Idara Maalum za SMZ.
Mh Masoud amesema sio vyema kuona tume hiyo inajiingiza katika mivutano na badala yake ihakikishe inatoa mchango mkubwa wa kuleta ufanisi katika utendaji kazi kwa Idara hizo.
Aidha ameitaka tume hiyo kutambua kuwa idara maalum zote ni kitu kimoja na ushirikiano kati yao ndio utakaofanikisha jukumu ya kusimamia vyema masuala ya kiutumishi.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Idara Maalum za SMZ Luteni Kanal mstaafu Mohamed Suleiman Ali, amesema atahakikisha wanafanyakazi kwa kuzingatia sheria ili iweze kufanikisha majukumu yake.