Wajumbe wa Baraza la Wawakili wameliomba Shirika la Umeme Zanzibar ZECO kuchukua hatua za ziada kwa kutafuta njia Mbadala linapotokea tatizo la kukatika kwa huduma ya Umeme
Wakichangia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji Nishati na Madini Wajumbe hao wamesema juhudi zaidi zinahitajika katika kutafuta mbinu nyingine za Nishati Mbadala ili kusaidia wakati wa kukatika umeme Ghafla
Kuhusu huduma za upatikanaji wa Maji Wajumbe hao wamesema bado Mamlaka ya Maji Zanzibar inakabiliwa na kazi ya ziada katika upatikanaji wa huduma hiyo kwa uhakika na kushauri kuvifufua Visima ambavyo vimeachwa kwa muda Mrefu
Wamesema upatikanji wa huduma hizo bado ni tatizo Sugu pamoja na jitihada zinazochukuliwa na Mamalaka hivyo ni vyema kuzitaftia Ufumbuzi wa Ziada huduma ambazo hazipatikani kwa muda Mrefu sasa